Mkutano huo ulihudhuriwa na
Mheshimiwa Janeth Mbene
Naibu Waziri wa Fedha Mheshimiwa Charles
Tizeba, Naibu Waziri wa Uchukuzi, MheshimiwaAggrey Mwanri Naibu Waziri, Ofisi
ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Mheshimiwa Gerson Rwenge
Naibu Waziri wa Ujenzi kutoka Tanzania
Katika
Hotuba za ufunguzi Wakuu wa Msafara kutoka Nchi Wanachama walisisitiza
uharakishaji wa utekelezaji wa Miradi ya kipaumbele iliyoanishwa na Wakuu wa
Nchi Wanachama katika Retreat yao ya pili iliyofanyika Jijini Nairobi mwezi
Novemba, 2012 iliyohusu Ufadhili na Uendelezaji wa Miundombinu.
Aidha
Mkutano huo ulipokea taarifa ya utekelezaji wa Miradi na programu mbali mbali inayotekelezwa
katika Nchi Wanachama. Katika kikao hicho ilielezwa kuwa ujenzi wa Vituo vya
pamoja Mipakani uko katika hatua mbali mbali za ujenzi na kwa upande wa Vituo
vya Namanga na Holili ujenzi unakaribia kukamilika na vituo hivyo vinategemewa
kufunguliwa rasmi wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama utakaofanyika
mwezi April, 2014.
Kukamilika
kwa vituo hivyo kutawezesha na kuharakisha usafiri na usafirishaji wa mizigo
miongoni mwa Nchi Wanachama kwa kuwezesha ukaguzi kufanyika upande mmoja wa
mpaka na hivyo kuharakisha ufanyaji wa biashara.
Mkutano
huo ulishuhudia mamlaka husika kutia saini Mkataba wa
Makubaliano wa utafutaji na Uokoaji (Memorandum
of Understanding on Search and Rescue), itifaki ya Afrika Mashariki ya TEHAMA
(Protocol for ICT net work) na Sera ya Afrika Mashariki ya taarifa za hali ya
Hewa (EAC Meteorological Data Policy).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...