Moses Kulola, muhubiri wa siku nyingi Tanzania wa kanisa la EAGT


Askofu Moses Kulola


Jabari la Injili, baba wa kiroho wa wengi, mtumishi anayejali wengine, amelala usingizi leo  1Thes 4;13-14, aliitwa na Bwana akiwa katika Hospitali ya AMI (African Medical Investment) iliyoko Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Moses Kulola alizaliwa mwezi Juni 1928, akitoka katika familia ya watoto kumi, watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule  ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.
Alimwoa Elizabeth na wamezaa  watoto10 ambapo saba bado wako hai na mmoja amebarikiwa kuwa mchungaji na mhubiri Pastor Daniel Kulola. Askofu Kulola alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa rasmi na Bwana mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa. 
Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wake serikalini ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea na kuingia katika kumtumikia Mungu. 



Mwaka 1964-1966 alisoma chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada yake. Hata hivyo aliendelea na masomo mbalimbali ya biblia ambapo alitunukiwa vyeti kadhaa kutoka mataifa mbalimbali.


alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 hadi 1991 ambapo alikuwa askofu msaidizi chini Askofu wa TAG wakati huo Askofu Lazaro na katika miaka ya 80 aliamua kuanzisha makanisa ya Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , DRC, Burundi,Malawi na nchi mbalimbali, kwasasa inakadiliwa kuna makanisa zaidi ya 4000 katika nchi kadhaa. 


 Kwa miaka zaidi ya 60 sasa  amekuwa akihubiri neno la MUNGU na licha ya umri wake amekuwa akihubiri na kuendelea kumtumikia MUNGU, katika hivi karibuni  katika viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam alihubiria maelfu ya watu na wengi walifunguliwa. 

Chanzo: SwahiliTV


Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola akipeana mkono na mwanae Daniel Kulola ambaye ni mchungaji. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.Amen

    ReplyDelete
  2. Mungu Mwenye Enzi ilaze Roho ya mtumishi wako mahali pema peponi. RIP Pastor Kulola. EEM

    ReplyDelete
  3. Huyu alikuwa zawadi kwa Tanzania kwa upande wa Injili kama Nyerere kwa upande wa siasa.Hakika kumpata mtu kama Kulola au Nyerere humchukuwa MUNGU miaka kuandaa mtu kama hawa.Jina la BWANA litukuzwe kwa haaya yote AMEN-Nnko documentarist wa Injili ya Kulola 1996-2000.

    ReplyDelete
  4. hili lilikuwa ni jembe la injili daaah asante MUNGU kwa kutupatia KULOLA,kiukweli umetupendelea,TUNASHUKURU.R.I.P BABA

    ReplyDelete
  5. Kweli nakubalia na mtoa maoni hapo juu. Mtumishi Moses Kulola alikuwa baba wa Injili nchini, amewalea wengi kiutumishi na amefanya vitu vya kitumishi ambavyo hayupo kwa sasa ambae anweza kusema kafanya zaidi yake. Nakumbuka hadidhi yake ya kutembea kwa mguu kutoka Njombe hadi Songea, sidhani kama kuna mtumishi mwingine nchini kafanya kitemndo kama hicho. Kitendo cha kutembea kwa mguu huku akiapiza ardhi anayoikanyaga kumrudia mungu, ni utumishi ulioifungua nchi.
    Wengi mtakumbuka kuwa ni miaka michache tu iliyopita nchi yetu ilikuwa imejaa giza kwa imani ya kishirikina, watu tuliishi kwa hofu kubwa ya kulogwa na kulikuwa na matukio yakutisha hususani huko vijijini lakini baada ya kazi nzuri ya kitumishi iliyofanywa na watumishi nchini ikiongozwa na Marehemu wetu Kulola, tumeshuhudia giza likiondoka na utiisho wa mungu ukitawala juu ya giza. Leo hii hatuna hofu tena ya uchawi wala waganga wa kienyeji wa kichawi.
    Kwa minajili hiyo, binafsi, kwa furaha kubwa nampongeza Marehemu kwa kazi nzuri ya utumishi wake nchini, namtakia mapumziko mema akingoja ufufuo ambao amekuwa akiuhubiri siku zake za mwisho wa safari yake.
    Naitakia Roho ya Marehemu Moses Kulola pumziko la amani ya Kristo milele.

    ReplyDelete
  6. R.I.P MOSES

    ReplyDelete
  7. Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi. Tutamkuka katika mahuribi yake alipenda kusema" " "Joooooo"Kuokoka ni lazima upende usipenda""Tusipoonana duniani tutaonana mbinguni" sasa hivi anashangalia na malaika.RIP Mzee Kulola"

    ReplyDelete
  8. Mtumishi wa mungu ambaye hakupenda fedha, hakujiinua,wala hakutegwa katika tanzu ya wanawake.Mfano wa kuigwa.

    ReplyDelete
  9. Jembe la injili Tanzania!He was a great man of God!I salute him

    ReplyDelete
  10. kweli Baba wa wengi kazi amemaliza naamini yuko kufuani mwaBaba yetu Ibrahim baba yetu wa imani. anasubiri taji na anazo nyingi,mtihani umebaki kwetu kumbe kila mtu anaondoka kama KULOLA kaondoka itakuwaje mimi tujioji sote.

    ReplyDelete
  11. YOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOoooooo. kwa heri babu.

    ReplyDelete
  12. Alikuwa baraka sanaa.kwa heli babu.by mama wa inno dar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...