Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Holland..Rais Shein yupo nchini Holland kwa ziara ya kikazi.
Balozi wa Tanzania nchini Belgium Mh: Diodorus Kamala akifungua mkutano uliojumuisha Watanzania wanaoishi nchini Holland kuzungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein hapo jana katika hotel ya Hilton iliyopo jijini Den Haag.
Mwenyekiti wa Tane nchini Uholanzi ndugu Kweba Bulemo akimkabidhi zawadi ya kitabu maalumu Mheshimiwa Rais Dr.Ali Mohamed Shein kama kumbukumbu alipofanya mazungumzo na Watanzania hao hapo jana nchini Uholanzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akitoa ufafanuzi wa maswali yote aliyokuwa akiulizwa na baadhi ya Watanzania kuhusu mustakabari wa Kisiwani Zanzibar
Pichani ni mahudhurio ya watanzania waliojitokeza kuzungumza na Mh:Rais Ali Mohamed Shein hapo jana katika ukumbi wa hotel ya Hilton


Asante sana kwa picha nzuri blog ya jamii.Kuchanganya Kiswahili na Kiingereza RUKSA kama kuna mtiririko mzuri(flow).Mfano Nchini Holland < nchini Uholanzi na nchini Belgium < nchini Ubeligiji.Hilo moja.La pili,nyie Watanzania mnaoishi huko Uholanzi "mnatesa" peke yenu tu?Naomba ufadhili na mimi nije kushangaa kidogo Amsterdam!Lakini nafuatilia habari za nyumbani(TZ),mnaelewa kinachoendelea hapa nchini kwetu kwa sasa?Nawatakieni wote WEEKEND njema.
ReplyDeleteDavid V
we anoy wa kwanza si kila siku mnasema sisi turudi maisha mazuri huko sasa ufadhili wa nini.
ReplyDeleteHaya alichokisema mbona hamtwambiii kuhusu ZNZ
Hongera kijana Mura Kweba(Mwenyekiti) kuzidi kutia fukuto la kuimarisha Umoja wa WaTz Hollannds. Bado kazi ya kuwajumuisha wengine zaidi ndo imeanza, funga libuti zaidi!
ReplyDelete