KCB Bank Tanzania, imekabidhi vifaa vya hospitali ambavyo ni oxygen flow meters venye thamani ya Tsh. 7,200,000/= kwa uongozi wa hospitali ya Mwananyamala
Huu ni mwaka wa pili mfululizo ambako benki ya KCB inatoa misaada kwa hospitali ya Mwananyamala. Mwaka jana tulitoa vitanda 65 vikiwemo 60 na loka zake kwa ajili ya wadi ya kinamama na vitano kwa ajili ya kujifungulia (delivery beds) vyote kwa ujumla vikiwa na thamani ya Sh. 45,000,000.
Hii ni kawaida ya KCB bank kutembelea vituo vyote ambavyo imepeleka misaada kila baada ya mwaka mmoja ili kuona manufaa yanayotokana na msaada husika. Ni matunzo na matumizi mazuri ya vifaa vinavyotolewa, yatakayoifanya benki ya KCB iongeze msaada au misaada kituo chochote kilichokwishasaidiwa, vivyo hivyo itakua hospitali ya Mwananyamala.
Tathmini ya mwaka jana inaonyesha benki ya KCB ilitoa misaada yenye jumla ya thamani ya Tsh 362,545,000/= katika mchakato ufuatao:
• Tsh. 145,024,000- Sekta ya Afya
• Tsh. 130,000,000- Sekta ya Elimu
• Tsh.73,521,000- Mafunzo kwa Wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs)
• Tsh. 14,000,000 - Sekta isiyo rasmi (jamii yenye shida mbalimbali kama vyakula, maafa n.k)
Mwaka huu KCB imetenga kiasi kikubwa zaidi cha fedha kwaajili ya kusaidia jamii inayotuzunguka katika sekta zilizotajwa hapo juu na mazingira nchini. Mikoa itakayofaidika ni pamoja na Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Morogoro na Zanzibar.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa tiba vya kuwekea mgonjwa gesi, vilivyotolewa na benki ya KCB kwa hospitali hiyo, Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa na katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye, akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani (kushoto), moja ya vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 7.2, vilivyotolewa na benki hiyo, vinavyotumika kwa ajili ya kumwekea gesi mgonjwa, Dar es Salaam Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk.Sophinias Ngonyani, akiangalia moja ya vifaa tiba vya kumwekea mgonjwa gesi, mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye (katikati), vifaa vilivyotolewa na benki hiyo kwa hospitali hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa,akimkabidhi moja ya boksi lenye vifaa vya kumwekea mgonjwa gesi, Mkuu wa Bima ya Afya wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Merina Nkullua, vilivyotolewa na benki hiyo, Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Oysterbay, Gladys Mhina, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya benki ya KCB, kuchangia madawati inayoitwa 'Buy 10 Get 90, ambayo benki hiyo itanunua madawati 90 na shule husika kutakiwa kununua madawati 10. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa
na katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB,Christina Manyenye.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...