Mgeni Rasmi katika Mpambano wa Kimataifa wa kuwani Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,kati ya Mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phil Williams wa Marekani,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangala (mwenye koti jeupe) akimvisha Mkanda wa Ubingwa huo,Bondia Francis Cheka baada ya kumshinda kwa Point Mpinzani wake,katika Mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Bingwa wa Zamani wa Masumbwi,Fransous Bhotha.
 Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kushoto) akimrushia makonde makali mpinzani wake,Phil Williams kutoka nchini Marekani wakati wa mpambano wao wa Kimataifa kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,uliofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Bondia Francis Cheka ameibuka kidedea baada ya kumchapa mpinzani wake huyo kwa Point.
Bondia Phil Williams kutoka nchini Marekani (kulia) nae alikuwa akijibu mashambulizi kwa mpinzani wake,Francis Cheka.hadi mwisho wa mchezo uliokuwa wa raundi 12,Francis Cheka aliweza kuibuka Kidedea kwa kumchapa mpinzani wake huyo kwa point na kufanikiwa kumnyang'anya mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU.
 Chukua hiyoooooo...
 Hapa lazima ukae,mie ndio kisiki cha mpingo:hivyo ndivyo Bondia Francis Cheka alivyoonekana kuifanya kazi yake vilivyo.
 Refa wa Mchezo huo akimzuia Bondia Francis Cheka baada ya kumkoleza makonde kisawasawa mpinzani wake,yaliyompelekea kwenda chini.
Mpambano ukiendelea.
Wanahabari wakipata taswira za mpambano huo.

VIDEO YA MCHEZO INAKUJA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Waandishi mnatakiwa muwekeze au makampuni yenu yawekeze katika kamera bora na za kisasa kuweza ku-'zoom'.

    Maana hiyo dizaini ya kukaribia mpigwa picha imepitwa na wakati. Hata ktk mchezo wa soka utaona waandishi kwa kukosa kamera za kisasa wanaamua kumfukuza kwa mabio mchezaji ili kupata picha, achene hizo.

    Mdau
    Wa-Twasira

    ReplyDelete
  2. hongera sana francis cheka, keep it up! ameshinda kwa point ngapi? vp mpambano mada maugo? tunaomba ripoti tafadhali.

    ReplyDelete
  3. Safi sana CHEKA! Huna Mpinzani kwa uzito wa kati Kg 75 dunia nzima.

    ReplyDelete
  4. Drill haiwezi kuzuia SMG (Francis Cheka)...

    ReplyDelete
  5. hongera zake ni jambo la faraja na la kujivunia kwa watanzania wote

    ReplyDelete
  6. Safi sana Cheka.

    Mdau wa Taswira mimi si muandishi wa habari lakani kwa mazingira ya mpambano kama huu, nadhani tatizo ni mwanga. Unaweza kuwa na camera ya kuweza ku zoom 100m lakini flash yako isiweza kutoa mwanga wa kukuletea taswira nzuri, hasa usiku.

    Michuzi hv lile darasa la kupiga picha lilikamilika? Maana kuna kipindi sikuwa ninakaa kwenye mtandao jpili.

    sesphy.

    ReplyDelete
  7. Raisi Obama tuletee mwingine huyu uliyemleta tayari Raisi Kikwete amempa mawe makali amesha mlaza chali!!!

    ReplyDelete
  8. Tanzania kwa Magumi tunatishaaa!!!

    Tanzania nyundo ya Chuma!

    Watanzania waliwahi kuhsuhudia katika Disco huko nchi za Ulaya Norway na Italy jamaa walikuwa dansini makundi ya Watanzania ikatokea jamaa mmoja wao akapata Demu wa Kizungu sasa muda Dansi limekwisha Wahuni wa Kizungu wakajifanya wana mind,,,ohhh zilichapwa kavu kavu Watanzania vijana wa Ki-Tanga waliwatwanga vichwa Wazungu chali, wakakimbilia Polisi walipikuja Polisi hawakuamini jinsi jamaa walivyo chanwa chanwa ktk nyuso zao n madamu kuwavuja walipigwa kwa vichwa na Watanzania na sio silaha!

    Nadhani Raisi Kikwete katika Michezo ni bora tubadili mwelekeo sasa tuje kwenye Ngumi kwa kuwa Mpira ni wazi hatuna chetu!

    ReplyDelete
  9. Asante sn KAKA cheka Moro tunatisha kwenye NGUMI,FOOTBALL,MUZIKI yani vipaji vya kumwagaa,mifano hiyo hapo,Hamisi Tobiasi GAGA (RIP)kwenye mpira wa miguu haitotokea mchezaji kama yeye,music mbaraka wa mwishehe (RIP),Afande sele,Stamina,Bele 9,Mc koba nawengineo kichele,naitwa mdudu KAKAKUONA mwenye macho ma3

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...