Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,  Dk. Makongoro Mahanga (kulia) akioneshwa mitambo ya kuzalisha majani ya chai katika Kiwanda cha Chai cha Luponde, wilayani Njombe, alipofanya ziara ya kutembelea viwanda na mashamba ya chai  pamoja na kuzungumza na wafanyakazi. Kushoto ni Meneja wa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Antony Mwai.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,  Dk. Makongoro Mahanga akionja aina jibini (cheese) zinazozalishwa na Kiwanda cha Maziwa  cha CEFA Njombe, wilayani Njombe, alipotembelea kiwanda hicho hivi karibuni.
 Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (kushoto) akizungumza na Meneja Biashara wa Kiwanda cha Chai Luponde, Athanas Mwasamene alipotembelea hivi karibuni  shamba la majani ya chai-dawa (herbal tea) wilayani Njombe. Dk. Mahanga alifanya ziara wilayani humo ambapo alitembelea viwanda, mashamba ya chai pamoja na kuzungumza na wafanyakazi.
 Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Chai Luponde, wilayani Njombe,  Anthony Mwai (mbele) akimwonesha Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (katikati), shehena za chai-dawa (herbal tea) zinazozalishwa kiwandani hapo, tayari kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi. Dk. Mahanga alifanya ziara wilayani humo ambapo alitembelea viwanda, mashamba ya chai pamoja na kuzungmza na wafanyakazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...