Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa akifungua
kongamano la Uchumi na Ajira kwa Vijana wa Tanzania lililofanyika katika ukumbi
wa Don Bosco jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kamati ya Kimataifa
ya Chama cha Convervative cha Denmark, Rolf Aagaaro-Svenevosen na Katibu Mkuu wa chama wa vijana wa chama hicho, Nicholas
Jansen.

Baadhi ya wafuasi wa Chadema wakinunua skafu, kofia za chama hicho wakati wa kongamano la Uchumi na Ajira kwa Vijana wa Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa akisalimiana na Katibu Mkuu wa chama hicho mrengo wa Vijana, wakati wa kongamano la Uchumi na Ajira kwa Vijana wa Tanzania lililofanyika leo katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Vijana wsakiwa katika kongamano hilo.
Katibu wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Deogratius Munishi akisisitiza jambo.

Nashangaa kuona leo wanajadili mambo ya maana,coz hiki chama sera zao wao nikuandamana tuuuu na kuwabuluza watakavyo vijana wa TAIFA la KESHO,,cc waona mbali tunataka mambo kama haya,,sio kila kukicha ooo usalama wataifa haufai mala polisi hawatupendi jamani tubadilikeni hata mambo ya kulinda nchi yetu aliyosema raisi wetu nijukumu letu sote,utaifa kwanza ndugu zangu na ndoa zote ambazo wageni wamewahadaa dada zetu ili wapate uraia wa kitanzania tunaiomba wizara ya mambo ya ndani ianze msako mkali sn usiku na mchana na watakao bainika hizo ndoa feki zivunjwe na waludishwe makwao,jamani tuikomboe nchi yetu ili iludi kama zamani asanteni watanzania wenzangu.
ReplyDeletewewe hapo juu, unatumia lugha ya kulaumu na ya kuudhi kuhusu CHADEMA, huwatendei haki. Kuna vitu vingi tusingevifahamu bila ya CHADEMA. wana sababu ya kuandamana kwa sababu hawatendewi haki, wanakandamizwa, wananyanyaswa na vyombo vya dola na serikali na msajili wana nia ya kuiididimiza. mbona ukweli utabakia ukweli siku zote?
ReplyDeleteNi kweli mdau wa kwanza ametumia lugha ya kuudhi japo ameuma na kupuliza, lakini leo hii laiti kama si hao unaowashutumu mengi tusingeyajua,kama ambavyo umesisitiza jukumu la ulinzi wa taifa ni letu sote na kuunga mkono ila uwe jaribu kuona mazuri pia ambayo ni mengi kwa upande wa pili.
ReplyDelete