Baada ya kuonyesha kiwango kikubwa kabisa katika mechi ya kirafiki kati ya Golden bush FC na Mwanza United uongozi wa Golden bush uko kwenye hatua za mwisho kabisa kukamilisha usajili wa beki kisiki George Magere Masatu mchezaji wa Zamani wa Pamba, Simba na timu ya taifa.

Mazungumzo ya kumuhamisha mchezaji huyo nyota kutoka Mwanza united yanafanywa na mwanasheria wa timu ya Golden bush FC bwana Godfrey Chambua  a k a Zacharia Hans Poppe. Bwana Poppe aliyeshikana mkono na Athumani Machuppa pichani ndiye aliyewezesha usajili wa akina Athuman Machuppa na Sadik Muhimbo ambao wote wametolewa kwa mkopo timu za Sweden na DRC.

Uwepo wa George Masatu kwenye timu yetu ya Golden bush veterans itaongeza chachu ya ushindi hasa ukitambua uwezo alionao bwana George. Tunawaomba wapenzi wetu wawe na subira wakati uongozi ukifanya kazi ya ziada kuahakiksha Masatu anatua Golden Bush  bila mizengwe.

Golden Bush kwasasa hivi wako camp wakijiandaa na game ngumu kabisa dhidi ya Pugu Veterans, game itapigwa Pugu kajiungeni siku ya jumamosi kuanzia saa mbili kamili asubuhi.  Tunalazimika kwenda kucheza pugu baada ya timu ya TASWA kuchomoa game ambayo ilitakiwa ipigwe siku ya jumapili uwanja wa Kinesi "ST James Park"

Imetolewa na msemaji na mchezaji mwandamizi wa golden bush FC

Onesmo Waziri "Ticotico"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Babuu leteni hiyo timu huku "R-chuga" kuna timu ya majombaa inaitwaga WAZEE WA KITAMBI NOMA..Nishida jamaa yangu!Mwanza veterans walikwepogo huku waka tarasuliwa mbaya!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...