Na Abdulaziz video,kilwa

Mbunge wa jimbo la Kilwa kusini Saidi Bungara (CUF) amelaani kitendo cha baadhi ya wananchi mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kukwamisha juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi kupitia uwekezaji wa gas ya asili nchini

Haya ameyaeleza kwenye hafla fupi ya kutiliana sahini mkataba wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nangurukuru kati ya halmashauri ya wilaya Kilwa na kampuni ya Afrikan Energy Inayojihusisha na utafiti wa mafuta na gesi.

Bungara alisema kitendo cha mwekezaji huyo kuwafanyia maendeleo wananchi wa wilaya hiyo ni ishara tosha ya kutambua michango na juhudi za wawekezaji katika kutoa huduma za kijamii kwa wananchi.

‘Kitendo cha mwekezaji wa pan African Energy kutoa misaada yenye lengo la kuboresha huduma za kijamii zimethihirisha ukweli wa serikali kuhusu faida na maana ya wawekezaji, sisiwa Kilwa hatuwaungi mkono wa Mtwara tuna sema itoke tu” alisema Mbunge Bungara.

Alisema watu wa kilwa hawana sababu kupinga ya kupinga uwekezaji wa namna yoyote kwani wanachohitaji ni maendeleo na sio vurugu na fujo kama wanavyofanya wananchi wa mkoa wa mtwara kupinga kuondoka kwa kesi .

Kwa upande wake Meneja wa huduma za jamii wa kampuni ya Pan Afrikani Energy Andrew Kashangaki alisema kampuni inafadhili ujenzi wa zahanati ya Nangurukuru na unatarajia kutumia zaidi ya shs milioni 234,714,980.

Kashangaki alisema sambamba na kusaidia ujenzi wa zahanati hiyo pia kampuni hiyo inalipa ushuru wa huduma ambapo hadi sasa imelipa kwa halmashauri hiyo zaidi ya shs milioni 638 na inatoa misaada mingine katika sekta ya elimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...