Wadu, 
Tunapenda kuwapa taarifa ya game muhimu kabisa siku ya jumapili asubuhi pale uwanja wa Kinesi (Shekilango) ambapo timu mbili maarufu za veterans yaani Golden Bush FC (mabingwa wa Jiji la Dar na mikoa jirani) na maveteran wa Mwanza united zitakutana uso kwa uso katika game ya kirafiki. ni mechi ambayo hutakiwi kukosa ukizingatia umahili wa wachwzaji wa timu zote mbili. 
Mwanza united ikiongozwa na wachezaji waliotamba sana katika timu za Pamba, Simba, Yanga na timu ya taifa, hapa tunazungumzia akina George Magere Masatu ambaye ndiye nahodha wa timu, Aaron Nyanda, George Nyanda, Emmanuel Swita, Benjamin Magadula na wengine wengi.
 Golden bush FC wameweka kambi Starlight Hotel Dar es salaam ili kuweka mipango ya pamoja ndani ya siku hizi mbili zilizobaki, pamoja na kuwa na wachezaji mahili sana kama Waziri Mahadhi Mandieta, Herry Morris, Wisdom Ndlovu, Nico Nyagawa, Juma Kaseja, Amani Simba, Amri Kiemba, Salum Swedi, Salum Athuman, Kudra Omary, Abuu Mtiro, Yahaya Issa Golden bush wanajivunia kuwa kikosi kikubwa kilichosheheni wachezaji hatari chini mwalim Madaraka Seleman “Mzee Wa kiminyio”.
 Uwanja uko chini ya ulinzi makili wa polisi na mgambo wa jiji ili kuepuka tabia wa wenzetu wa mwanza kutumbukiza vitu vyao vya kishirikina.
 Karibuni sana mje mpate burudani ya kukata na Mundu.
 Ally Mayay ndiye atakuwa mwamuzi wa game hiyo.

Imetolewa na msemaji wa timu 
Onesmo Waziri “Ticotico”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...