Kamati ya Hesabu za Serikali imekutana na Wizara ya Ardhi kwa madhumuni ya kupitia Hesabu za Wizara kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 2012. Changamoto za Wizara ni nyingi sana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amehoji mambo mengi sana na mengi ni wizi, upotevu wa mapato ya Serikali na malalamiko ya wananchi kuhusu ardhi. CAG alitoa hoja za ukaguzi maeneo ya mapato kutokusanywa, kulimbikizwa na hata kukusanywa bila kuyawasilisha Wizarani.

Katika Mwaka wa Fedha 2011/12 Wizara ilipangiwa kukusanya jumla ya Shilingi bilioni tisini na tisa (99 bilioni) lakini ilikusanya shilingi bilioni ishirini tu (20 bilioni) sawa na asilimia 21 ya makadirio.

CAG pia alihoji masuala ya viwanja vilivyopimwa, kugawiwa watu lakini watu hawakupewa hati ambapo zaidi ya viwanja 7, 342 vilikutwa ni viwanja vyenye shaka. Pia viwanja 160 jijini Dar es Salaam vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 555.8 milioni viligundulika ni viwanja ambavyo walijigawiwa maafisa wa Ardhi maana haoakuwa na ushahidi wowote wa mauzo ya viwanja hivyo. Hoja nyingine ni pamoja na ukiukaji wa sheria kwa kujengwa kwenye fukwe nk.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Zitto, we believe in you...and we believe in the changes that you can bring to out country...ZITTO ni barack wetu wa Tanzania...Change we can believe in...Zitto PLEASE do not stop and do not leave any stone unturned...fukua kila mahala..mpaka kieleweke

    ReplyDelete
  2. May god bless all who have true love to this country.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...