Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek Namibia.

Wanariadha wanaowakilisha Jeshi la Polisi Tanzania katika michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika SARPCCO nchini Namibia wameanza vyema mbio hizo baada ya kufanikiwa kunyakua medali za Dhahabu na fedha katika mbio za mita elfu 10000 wanaume.

Aliyenyakua medali ya dhahabu ni Mwanariadha Fabian Nelson ambaye alitumia dakika 30 na sekunde 42 huku akifuatiwa na Wilbrado Peter (Tanzania) ambaye alitumia dakika 30 na sekunde 45 na kuwaacha wanariadha wengine nyuma kutoka mataifa ya Zimbabwe,Namibia,Botwasana na Angola.

Wengine walioipatia Tanzania Medali ni pamoja na Basili John mita 800 (Shaba ) na Mohamed Ibrahim mchezo wa kurusha kisahani (shaba).

Katika mpira wa miguu mechi ya ufunguzi ilizikutanisha wenyeji Namibia na Msumbiji ambapo Namibia iliichapa Msumbiji mabao 2 kwa 0 huku kwenye mpira wa miguu wanawake Namibia na Angola zilitoka suluhu ya bila kufungana.

Tanzania itaanza kutupa karata yake katika mpira wa miguu dhidi ya Zambia ambapo Tanzania imepangwa kundi B ikiwa na timu za Zambia, Angola ,DRC na Lesotho huku Kundi B lina timu za Namibia, Msumbiji, Botswana na Zimbabwe.
Mbio zikiendelea
Mwanariadha Fabian Nelson akivishwa Medali ya Dhahabu baada ya kushika nafasi ya kwa katika mbio hizo,ambapo alitumia dakika 30 na sekunde 42 huku akifuatiwa na Wilbrado Peter (Tanzania) ambaye alitumia dakika 30 na sekunde 45 na kuwaacha wanariadha wengine nyuma kutoka mataifa ya Zimbabwe,Namibia,Botwasana na Angola.
Furaha ya ushindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hongereni sana na asanteni kwa kuliletea taifa heshima.

    ReplyDelete
  2. Polisi Tanzania Nyundo Kubwa!!!

    Ohhh mnakamata kila kona hata nje ya Tanzania?

    ReplyDelete
  3. Polisi Tanzania.

    Waambieni huko kwenye Mashindano Namibia kuwa huku Tanzania Polisi inaitwa NGUNGURI!!!

    Mdau mwenye neno NGUNGURI kwa Lugha ya Kiingereza tafadhali tuhsukie hapa kw ajili ya watu huko wasiojua Kiswahili.

    IGP Mstaafu Mzee Mahita upo apo?

    ReplyDelete
  4. kwa nini wakimbiaji hawa wa mita 10,000 hawakwenda Moscow 2013 world champions?

    ReplyDelete
  5. wakimbiaji hawako kusini mwa afrika. kama wako fiti wakashindane na wakenya na waethiopia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...