Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akilakiwa na baadhi ya Majaji na Wanasheria kutoka Tanzania na kwingineko Afrika, anayesalimiana naye ni Mhe. Jaji Sanji Mmasenono Monageng, ambaye ni Makamu wa Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Kihalifu (ICC), na Kamishna wa International Commission of Jurists, anayefuata mwenye koti refu jekundu ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Jaji Eusebia Munuo, Kongamano hilo limefunguliwa mapema Leo na Jaji Mkuu katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) akiwa katika meza Kuu na viongozi wengine wa Mahakama, kulia ni Mhe. Jaji Mstaafu, Eusebia Munuo, anayefuata ni Mhe. Jaji Sanji Monageng, Makamu wa Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Kihalifu (ICC), wa pili kutoka kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wa kwanza kushoto, Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania
Baadhi ya Majaji wanawake wakiwa katika Kongamano hilo tayari kwa ufunguzi rasmi.
Jaji Mkuu wa Tanzania katika picha ya pamoja na Majaji Wanawake kutoka nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Naigeria, Zambia, Swaziland, Zimbabwe, Botswana, Msumbiji, Namibia, Sierraleone, Eritrea, Lesotho, Mauritius na Malawi. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania).
Naona kama kuna wanaume ktk mkutano wa wanawake au macho yangu mabovu?
ReplyDelete