Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais Joyce Banda wa Malawi muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lilongwe tayari kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC leo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtoto muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lilongwe tayari kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana nawakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama muda mfupi baada ya kuwasili Lilongwe Malawi kuhudhuria Mkutano wa SADC
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Rais Joyce Banda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lilongwe tayari kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC leo.
Picha na Fred Maro






"...Umeona suala la mpaka wetu lilivyo la kihistoria mama..!!? Ndivyo Rais JK anavyoonekana akimwambia Rais wa Malawi JB katika picha ya kwanza kutoka chini.
ReplyDeleteDavid V
Hapo kila mmoja anawaza Ziwa Nyasa,wanacheka usoni tu lakini kila mmoja anasubiri mwenzake aanzishe isaue
ReplyDeleteWatu wa mitandao ya jamii kwa kukuza mambo , oneni sasa Wakuu wa Nchi wanacheka kwa tabasamu la ukweli.
ReplyDeleteNawaomba wadau wa mitandao ya kijamii na wahariri wa magazeti kuwa makini na michango yao kuhusu uhusiano kati ya Tanzania na nchi -majirani .
Mdau
Makini
Ivi ngoma za jadi ni sie tu ndio tuliojaaliwa vipaji?Sioni tarumbepa hapo du!na mdau wangu wa matarumbeta nae pia atakua anajiuliza.
ReplyDeletena hii (SADC) ndio jumuiya ya ukweli ambayo haina unafiki wala ajenda ya siri. Siyo kama ile nyingine. Mijitu unaisaidia lakini haisaidiki. Unawapa mawazo ya kutulizana, wao wanakuona mbaya. Kauli ya Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,nanukuu; "Katika jamii hii, watu wapo katika sampuli nyingi, sampuli nyingine, mazingira ya utulivu hayawapi raha, wanajiuliza kumetulia, kwa nini kumetulia?" Nimenifurahisha na hao jamaa wanatakiwa iwaingie mioyoni mwao na waifanyie kazi, na sio kujenga chuki zisizokuwa na mpango.
ReplyDeleteTanzania sasa hivi tunatakiwa tujikite zaidi na SADC maana hii EAC ni majanga matupu...huko SADC tunaheshimika na nchi zinaheshimiana sio hawa EA wako sana kwa maslahi yao ya kuja kutunyonya na kuchukua ardhi yetu..tulishajifunza kosa ilipovunjika EAC 1977...tusirudie kosa plzz mh. rais JK ..hebu pitieni tena mkataba wa EAC ikibidi tujitoe mapema...kurudia kosa never!
ReplyDeleteHuyo 'mdada' hana amani kabisa moyoni kwani hilo tabasamu analazimisha tu wallah!
ReplyDeleteMhe. Raisi JK mweleze huyo mama Ziwa Nyasa halipati ngo' kwanza lina Mafuta na Gesi na sisi tumesha saini Mikataba na Obama.
ReplyDeleteKama anataka Ziwa Nyasa mwambie nchi yake Malawi ijiunge na JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA halafu iwe Mkoa na yeye awe Mkuu wa Mkoa wa Malawi!!!
Raisi Jakaya Kikwete ndugu yetu ni wakati sasa wa kuimarisha Vikosi vya Majeshi Mpakani na Malawi!
ReplyDeleteMimi na Watanzania wengine wengi tu Makini tupo tayari kutumikia Jeshi na nchi kwa Vikosi hivyo kwa kupitia Mpango wa Linda nchi wa JKT!
Ohooo ukubwa ni jiwe!
ReplyDeleteHuyo mama usoni anaonyesha yamesha mshinda anatamani arudi Jikoni akapike!, amepigania kudai Ziwa Nyasa anaume na Vigogo wa Siasa na Diplomasia za Kimataifa kama Mhe.Raisi JK na Nguli Mhe. Bernard Camilius Membe kakabiliana na Wanaume weee kamasi zimemtoka na sasa amekoma.
Uraisi mchezo?
hahahaha!
ReplyDeleteMdau wa 7 huyo 'mdada' hana amani kabisa moyoni kwa vile ni wazi amekoma!
anajua amesha onga ukuta kubishana na Kikwete Mzee wa kazi.
Joyce Banda amekona kwa Raisi Kikwete kwa mengi tu.
ReplyDeleteKwa kweli isije ikatokea ukaja kumchukia mtu aliyekuzidi kwa mengi, utaumia sana!...ni sawa na kupiga ngumi ukutani ni kuwa utaumia mwenyewe!...au ni sawa na kugombana na kivuli chako mwenyewe!.
Haya matatu (3) hapa chini yatakuwa yanauchoma moyo wa mama Joyce Banda laiti kungekuwa na kifuniko tukafungua tungekuta moyoni mwake kuna mambo haya:
1.Tanzania na Marekani imesaini mikataba ya uwekezaji wa Nishati alipokuja Brother Big Obama Julai mwaka huu wakati Ziwa Nyasa lina Mafuta na Gesi...hiyo ina maana yeye ndio ameula wa chuya hana chake akileta nyoko atashuhudia Madege ya Marekani angani na Madege ya siyo na Marubani ya Drones.
2.Raisi Kikwete ametinga na ndege ya Uraisi ikiwa na ADAMU NA HAWA yetu ya tena ikiwa inag'ara kama dhahabu ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA wakati yeye uwezo huo akisafiri hana nchi yake masikini inapumulia mashine anatumia ndege za Mashirika ya Kibiashara!
3.Ameshajua wazi mama Joyce Banda ya kuwa Ziwa Nyasa ameshalikosa!
Kwa kweli ninafarijika nikiona vitu hivi hapa vitatu:
ReplyDeleteNinapomuona Raisi wetu Mhe. Ndugu JK akiwa ktk ndege maalum ya Raisi ikiwa na vitu vitatu:
1.Nembo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Adamu na Hawa).
2.Jina TANZANIA
3.Yeye mwenyewe akiwa ameshuka ktk dege hilo.
Kwa kweli hayo matatu kama Mwana wa Tanzania yananifaya nipate matumaini na nifarijike saaana!
Kama hapo anakutana uso kwa uso na hasimu wetu mkubwa Tanzania mama Joyce Banda!
Mungu ibariki Afrika ,
Mungu ibariki Tanzania!
Macho yanacheka ohhh Moyo unalia!
ReplyDeleteNikilikumbuka Ziwa Nyasa nililolikosa, nikilikumbuka aaah Ziwa Nyasa nililolikosa
Macho yanacheka ohhh Moyo unala X 3
Talalalala , tantalila, talalalala, tantalila.
...................................
Huo ndio wimbo unaooneka kuwa moyoni mwa Raisi wa Malawi Joyce Banda.
Wadau kucheka na kulia ni sawa?
Wadau unaweza kulia huku ukiwa unacheka?
Hali hizo mbili ndio zinazomtokea Mamie Raisi wa Malawi!
Ni kuwa ana kilio moyoni lakini anajilazimisha kucheka !
Sasa mwisho wake anabaki na uso wa sinto fahamu kama mnavyo muona hapo, ni kuwa anahitaji asicheke andelee na Kilio !
Mweleze huyo mama Ziwa Nyasa hapati ng'o!
ReplyDeleteWinner and Looser!
ReplyDeleteWinner is always Smiling, while Loose is always Crying!
Over the Lake Nyasa dispute Hon. Kikwete is the Winner that is why he is smiling while the Crying faced Madame Joyce Banda she is the Looser !
Dr.Kikwete,
ReplyDelete1.Umeshatoa Masomo kwa ndugu yako Paul Kagame kuhusu jinsi atakavyoweza kuondoa tofauti na Majambazi wa Vita na Waasi na nchi yake ikawa na amani.
2.Na huko Malawi mpe Mafunzo yako ya Uchumi mama Joyce Banda ya kuwa atumie sehemu ya maji yake ktk Ziwa Nyasa kwa Tija ili anufaike Kiuchumi na kutumia kwa nchi yake sio adai Ziwa Lote liwe la kwake!
Asilete Joyce Banda ule mtazamo wa Kitoto mkiwa mnakula pamoja mmoja akataka ugali wooote ktk sahani na bakuli la mboga viwe vya kwake!
Mkumbushe ya kuwa Afrika ni moja.
Mwanamuziki Mrisho Mpoto ameimba ''akufunzaye usikombe mboga anataka ushibe''
Joyce Banda utakoma kulinga na utaijua Tanzania!
ReplyDeleteheheheheheeee!!!!
ReplyDeleteKwa kweli nimecheka kwa maoni kuhusu Raisi wa Malawi Mama Joyce Banda mpaka basi!
Ndio maana nchi zingine kama Burundi, hata huko Malawi,Kenya na Zambia Mtanzania hapelekwi na kupandishwa Kizimbani Mahakamani.!
Ni kuwa akiambiwa ajitetee akijieleza ni lazima ATAKUWA HANA HATIA ! ATACHOMOKA !
Ehhhh Mama Banda ana simanzi hadi usoni anaonyesha ni vile amesha zidiwa 'Mizungu' kotekote kila Idara na wenye kuyajua mambo akina Kikwete na Membe!
Halafu kubwa la tukio wote wawili Mhe. Kikwete na Mhe.Membe wapo ndani ya mjengo Lilongwe!
Kweli panatosha hapo?
Ndio vile mamie JB amesha zidiwa 'Mizungu'
Enhee Mdau wa 19 juu,
ReplyDeletekama Mtanzania hapandishwi Kizimbani Malawi,Burundi,Kenya na Zambia ndio Mtuhumiwa anapelekwa Jela moja kwa moja bila kupitia Kesi Mahakamani?
Watanzana wanajua kuongea si mchezo!
ReplyDeleteKwa Vijembe?, ohhh balaa!
Nashauri Maoni haya apelekewe Raisi Joyce Banda mwenyewe aone!