Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo akitoa maelezo ya awali kabla
ya kumkaribisha Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe(hayupo pichani)
kufungua mkutano wa kwanza wa kamati ya Uendeshaji ya Matokeo makubwa sasa katika sekta ya
Uchukuzi, leo katika ukumbi Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Wajumbe
wa kamati ya Uendeshaji ya Matokeo Makubwa sasa (Big Result Now) ya sekta ya
Uchukuzi wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe(hayupo
pichani), wakati Waziri huyo alipofungua mkutano wa kwanza wa kamati hiyo leo katika ukumbi wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kulia), akisisitiza jambo wakati
wa mkutano wa kwanza uliowakutanisha wajumbe wa kamati ya uendeshaji ya Matokeo
makubwa sasa(Big Result Now) kwa sekta ya Uchukuzi, wakati alipokutana na
kamati hiyo leo mchana katika ukumbi wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Kulia kwa Waziri Mwakyembe ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Gerson Lwenge.
Kushoto kwa Waziri Mwakyembe ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kusimamia
utekelezaji wa Matokeo makubwa sasa iliyopo chini ya Ofisi y Rais, Bw. Omar
Issa.
Mratibu
wa Miradi iliyo kwenye mpango wa Matokeo makubwa sasa katika sekta ya Uchukuzi,
Bw. Aunyisa Meena akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa
kamati ya Uendeshaji katika sekta ya Uchukuzi, leo mchana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli(RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito
akifafanua hatua iliyofikiwa kwenye miradi ambayo iko kwenye Mpango wa matokeo
makubwa sasa katika sekta ya uchukuzi, wakati wa mkutano wa kwanza wa kamati ya
uendeshaji katika sekta ya Uchukuzi,uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa
Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam. PICHA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINII UCHUKUZI


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...