Mwanamuziki
kutoka nchini Uganda

Usiku
huo wa Chameleon utaenda sambamba na burudani kali kutoka kwa MA DJ wakali, DJ
Pac na DJ Senorita ambao watafanya show ya utangulizi.
Akizungumzia
burudani hizo, Meneja Uendelezi wa Biashara wa Escape Complex, Anthony David,
alisema watu watarajie burudani kali siku ya jumamosi hasa kwa kuwa sherehe hizo
zitaenda sambamba na sherehe za Eid za pale Escape Complex.
‘Kama
lilivyo jina lake, Escape ni mahali ambapo mtu anakuja kupumzika kukwepa
mihangaiko ya kila siku, iwe kikazi au kimaisha, lakini Eid hii tumeandaa
burudani hii ili kuwapa wakazi wa Dar es Salaam kitu tofauti’ anasema Anthony.
Mbali
na Chameleon siku ya jumamosi, Escape Complex imeandaa burudani siku ya Eid Mosi,
ambapo DJ maarufu Boni Luv atatoa burudani kali, na siku ya Jumpili, bendi
inayokuja kwa kasi Skylight, itawaburudisha wapenzi wake kuanzia asubuhi ili
kuimaliza wikiendi ndefu.
Escape
Complex, ambayo ipo Mikocheni/Kawe karibu nyuma ya ukumbi wa Safari Carnival,
ni Club mpya ambayo inapendezeshwa na ufukwe pamoja na mandhari ya kuvutia,
pamoja na chakula kizuri kwa wateja wake.
Mashabiki
wa Chameleon watalipia shilingi elfu kumi na tano ili kuburudishwa na
mwanamuziki huyo mashuhuri. Na VIP watalipa elfu 40,000/= ikiwemo kinywaji cha
bure pamoja na nafasi ya kumuona msanii huyo baada ya maonyesho.
Si tulipatana asikanyage ardhi hii?nani kasaliti?
ReplyDeleteWatu wengine kwa kutaka hasara,kuvuma kote kule bado wataka kujaribu bahati yako?haya yetu macho.
ReplyDeleteShigongo si ulikuwa unamdai huyu Chameleon?Time ya kumkamata ni sasa. Za mwizi arobaini.
ReplyDeleteUkweli ni kwamba ana kipaji,fikiria muda aliokaa kwenye chat,tofauti na wasanii wengine wa kukopi na kupesti nyimbo za Wanigeria na wasauz,sijui kwanini kina Joti wamekaa kimya
ReplyDeleteMdau wa Kwanza:
ReplyDeleteHata mimi nashangaa kuona hili Tangazo wakati radhau aliyotuonyesha huyu jamaa Mganda sikutegemea kama atakanyaga TZ!
OK, wacha ajaribu bahati yake tena kama Mdau wa Pili anavyonena kwa kuwa mwenyewe amehangaika wee dunia nzima hadi California Marekani alikwenda mwezi uliopita lakini amekuja kutambua kuwa Bongo ni MBUYU WA STAREHE hivyo ameona arejee tena!
Wewe Mwandaaji nadhani mngefanya mpango wa kuandaa Msamaha ama jamaa atoe FREE STYLE moja ya Wimbo kuwa surprise na kuwaangukia kwa kuwaomba Msamaha Watanzania!
Mdau wa kwanza umevunja mbavu zangu
ReplyDelete