Na Francis Godwin
HUKU kukiwa na taarifa ya baadhi ya wanahabari mkoa wa Morogoro ambao wanadai kushindwa katika uchaguzi wa klabu yao kuanza mchakato wa kuanzisha klabu yao mpya ,uongozi wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) umetoa onyo kali kwa klabu ya moja morogoro Press klabu kuwa kamwe klabu hiyo hakitatambuliwa na UTPC itakuwa ni klabu ya wanahabari wa vijiweni.
Tamko hilo limetolea mjini Dodoma leo na Mkurugenzi Mtendaji wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan wakati wa mkutano mkuu maalum wa kupitia rasmu ya katiba mpya ya UTPC .
Bw Karsan alisema kuwa amepokea taarifa kutoka mkoa wa Morogoro kuwa kuna baadhi ya viongozi wa klabu hiyo ambao walishindwa kwenye uchaguzi uliowatoa madakani.
" UTPC inatoa onyo kali kwa wanahabari wanaoanzisha klabu hiyo ya moja morogoro Press Klabu kwani hadi sasa kwa katiba ya UTPC kila mkoa unapaswa kuwa na klabu moja pekee na kwa mkoa wa Morogoro tunatambua klabu ya Moro Press klab pekee si nyingine ....hatuwazuii kuendelea na mchakato ila sema hiyo klab yao itakuwa ya kijiweni haitatambulika kamwe na UTPC"
Bw Karsan alisema kuwa wapo baadhi ya wanahabari wanaondolewa katika vyama vyao vya msingi kwa kwa utovu wa nidham na kukimbilia kuanzisha klabu za uchochoroni ambazo kamwe hazitatambuliwa .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...