MFUKO wa vyombo vya habari nchini TMF umefanya ziara ya kutembelea
katika kijiji cha Chekereni kilichopo wilaya ya Moshi vijijini
kujionea hali ya uchafuzi wa maji katika mto Karanga yanayodaiwa
kuwaathili wakazi wa maeneo hayo.
Afisa tathimini na ufuatiliaji wa mfuko wa vyombo vya habari nchini
TMF Sanne van den Berg alifika katika maeneo mbalimbali ya mto huo
kujionea hali hali hali ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wakazi wa
maeneo hayo wakiwemo viongozi wa kijiji.
Hatua hiyo imefuatia kutolewa taarifa za uchafuzi wa maji katika mto
huo unaofanywa na baadhi ya viwanda vilivyoko jirani na mto huo na
kusababisha madhara kwa wakazi wa vijiji vilivyoko kando ya mto huo.
Afisa tathimini na ufuatiliaji wa mfuko wa vyombo vya habari nchini
TMF Sanne van den Berg akiongea na mmoja wa wakazi wa kijiji cha
Chekereni alipotembelea mto Karanga kujionea uchafuzi unaofanyika.
Sehemu ya mto Karanga iliyomeguka ikiwa jirani kabisa na nyumba
zilizojengwa kando ya mto huo.
Sehemu ya kuhifadhia maji machafu kabla ya kuelekezwa mto Karanga,maji
yanayotoka kiwanda cha karatasi cha Kibo ambayo hata hivyo sehemu hiyo
inaonekna haitumiki .
Afisa tathimini na ufuatiliaji wa mfuko wa vyombo vya habari nchini
TMF Sanne van den Berg akipita katika daraja lililopo jirani kabisa na
eneo kunako fanyika uchafuzi wa maji .
Sehemu ambayo uchafuzi wa maji ya mto Karanga kama inavyoonekana .
Afisa tathimini na ufuatiliaji wa mfuko wa vyombo vya habari nchini
TMF Sanne van den Berg akiongea na mwenyekiti wa kitongoji cha Relini
Sadick Kubingwa alipomtembelea nyumbani kwake kuzungumza naye kuhusu
uchafuzi wa maji mto Karanga.
Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...