![]() |
Chissano John Nindi
Leo tarehe 28 augusti ni mwaka mmoja (1) kamili toka ulipotutoka bila neno la kwaheri.Chissano,uchesi uliokuwa nao unadhihirishwa na hii picha yako.Ulikuwa ni mpenzi wa kila mtu kwani ulithamini utu wa mtu.
Ni vigumu kuamini kuwa ni kweli haupo nasi.
Kazi ya Mungu haina makosa. Tukijiuliza sana kwanini alikuchukua wakati tulikuwa tunakuhitaji sana tutakuwa tunakufuru. Tunajaribu kujifariji kwa kuamini kuwa alikuchukua kwavile alikupenda zaidi yetu. Tunajitahidi kujiridhisha kuwa huko ulipo unapata pumziko la amani. Japo haupo nasi kimwili tupo nawe kiroho siku zote.
Unakumbukwa na ndugu zako wote,jamaa na marafiki zako.
Bwana alitoa na bwana ametwaa,jina lake lihimidiwe,amen. PUMZIKA KWA AMANI CHISSANO NA TUTAKUKUMBUKA DAIMA. |
Home
Unlabelled
KUMBUKUMBU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



RIP Chissano, nakukumbuka SUA na uchesho wako. Kyaruzi - BVM
ReplyDelete