Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma leo, Agosti 25, 2013. Kikao hicho kilifanyika kwa ajili ya kukutana Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera, Constansia Buhiye, Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Abedi Mushi, Mwenyekiti na Katibu wa CCM wilaya ya Bukoba mjini na Meya wa Manispaa ya Bukoba Anatory Amani, kuhusu mgogoro wa madiwani wanane wa CCM Manispaa ya Bukoba. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Ndugu Constansia Muhiye na Katibu wa CCM wa mkoa huo,Ndugu Abedi Mushi wakisubiri kuingia ukumbini kukutana na Kamati kuu mjini Dodoma leo.
Mbunge wa Bukoba mjini Mhe Khamis Kagasheki akiwasili Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Ndugu Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini Mwana-CCM mwenye ulemavu wa miguu, Shija Luhende kutoka Mwanza, ambaye alimkuta kwenye viwanja vya Makao Mkuu ya CCM mjini Dodoma leo, akitafuta msaada wa baiskeli.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Abdallah Bulembo akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,  Ndugu Jenista Mhagama, nje ya ukumbi, Makao Mkuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Picha na Bashir Nkoromo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. lssa ilijimbo hakuna cha ccm wala nini bila kagasheki, huwezi kuona mbuge au hata hao madiwani wa ccm, na bila kagasheki huyo mganda amani hata udiwani asinge upata, sasa waache hao watu wa ccm wamkumbatie waje waone cha moto kagasheki anasaidia kila mtu njoo bk uulize watu watakwambia makanisani misikitini pote anasaidia, lakini ccm haipendagi watu wachapa kaz.

    ReplyDelete
  2. Thubutu na wangeona cha mtema kuni!Wangejipindua kidogo tu kuwafukuza,wangechekea chooni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...