Ubomoaji wa moja ya majumba kadhaa makukuu katika mtaa wa Samora jijini Dar es salaam umeanza leo jioni na kuendelea hadi usiku kupisha ujenzi wa majumba mapya ambayo hapana shaka yatabadilisha taswira ya mtaa huo ulioanzaa kwa jina la Acacia na baadaye Independence na sasa Samora. Ripota wa zamu katika doria ya sikuu anasema zoezi hilo linaendelea kwa amani na usalama chini ya ulinzi mkali wa polisi
 Bomoa bomoa ya majumba ya Samora ikiendelea
 Jumba mojawapo likipigwa nyundo
 Ni usiku wa saa nne na zoezi linaendelea
 Mlinzi akiwa kasimama kidete kuhakikisha zoezi linaendeshwa bila rabsha
 Taswira ya eneo la tukio, jirani na iliyokuwa mgahawa wa Salamander ambao nao umeshazungushiwa uzio baada ya kupigwa nyumndo kitambo
Taswira ya mtaa wa Bridge street

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. JAMANI JAMANI, TANZANIA MUWE MNAFIKRA ANGALAU KIDOGO. WAPI TUNA ENDA NA WAPI TUILOTOKA?

    SASA HISTORY ITAKUWEPO WAPI HAPO `? THE COMING GENERATION ITAAMBIWA VIPI WAPI ILIKUWA DAR SE SALAAM?

    HIO TAASWYRA MPYA MNAYOISEMA NINYI NI KUITU GANI KAMA MJI UNATAKIWA KUWA MPYA BADO SEHEMU NI NYINGI SANA AMBAZO HAZINA MAJENGO KAMA TUNATAKA ENDELEZA MJI WE HA VE TO MAKE THE NEW DAR, SIO KUVUNJA VYA ZAMANI KUJENGA UPUUZI HAO WATALII WATAKUJA ONA NEW BUILDINGS?

    ATI TUNA WASOMI ! HUO MJI AU SAMORA YETU NI TREASURE NDIO KIVUTIO CHA KUJIVUNIA SASA NAONA WOTE SWAIN

    ReplyDelete
  2. Yani machozi yananilengalenga nikisoma habari kama hizi, hii ni historia yetu ambayo tunahitaji kujifunza, kuitunza na kuienzi.
    Jamii inayosahau historia yake, haina cha kufundisha vizazi vipya na mara zote hujikuta inarudia makosa.
    Architecture na hand detail ya haya majengo hakuna tena dunia nzima, watu wanasafari mbali kuona na kujifunza kuhusu kipindi hichi cha historia.
    Wawekezaji wanatakiwa kupewa maeneo mapya ambako itabidi wavute maji, umeme na kuleta maendeleo ya kweli sio kutumia miundo mbinu yetu ya zamani ambayo wananchi walishalipia kwa namna za to faulty.

    ReplyDelete
  3. Oh dear! Oh dear! How very sad. Kwa kweli historia ya DSM inapotea. This should be a 'listed building'. A few refurbisments ingetosha kabisa. Nasikia uchungu sana. Kwanini wasijenge sehemu nyingine? Kwa mfano kuanzia pale Namanga hadi Tegeta. Expand the city.

    ReplyDelete
  4. Yaani this is so sad...Salamander, a place tulikuwa tunapelekwa once a year kul Ice Cream..Kristmas time....I think hata ndipo BF wangu wa kwanza alinitoa out hapo. Kweli hatuwezi kuyahifadhi haya majumba? Wenzetu wanaitwa "Historical Places/Houses" siye tunaita "Majumba makuukuu"???

    Kesho na keshokutwa watabomoa shule ya Forodhani na Kanisa kama lile la St. Joseph manake nayo ya zamani.....

    Heee kweli uzee kumbe dhambi....

    ReplyDelete
  5. Histor class bwana.....let dem gooo introduce new city

    ReplyDelete
  6. Nimesikitika sana! Sasa nimeamini wasomi wote wamekimbia nchi, huu ni ujinga wa hali ya juu. Hatuthamini vya kwetu, tunakimbilia kugeza vya wenzetu. Haya sasa endeleeni kuishusha thamani ya Tanzania, uaneni kwa mi range rover na nguo za ku import, wamwagieni wageni tindikali, na endeleeni kushindana katika mavazi bila kusahau kuimba nyimbo za mapenzi za kukopi na ku pesti! Aibu sana.

    ReplyDelete
  7. Hivi jamani watoto wetu watajifunza historia ya maisha yetu kutoka wapi? Dar es salaam ina maeneo mengi ya kuendeleza mji, mfano kigamboni ingeitwa modern city na waiache city centre, wakarabati majengo hayo, iwe old town. Kinaweza pia kuwa kivutio cha watalii. So so sad!

    ReplyDelete
  8. Embu na nyie mnaopinga maendeleo acheni ufala. Nani kakwambia historia inamlisha mtu. Huko Uingereza kwenyewe kwenye conservatives original wanavunja majumba makuukuu kupisha mapya, hasa hasa yanayokuwa mazee na yenye kuhatarisha usalama wa watu kama hayo ya samora. yaani tanzania imegeuka nchi ya wabishi na wajuaji sasa. na kilka mtu anamwona mwenzie mjinga ila yeye anajua sana. acheni umbumbumbu nyie watanzania wachache

    ReplyDelete
  9. naungana mkono na mdau hapo juu. nimetembea miji mikuu yote afrika mashariki na ughaibuni sijaona magofu katikati ya mji. tatizo wabongo wajuaji wa kiiiilaaaa kitu ndioo maana kila kitu ni ubishi tu. tembeeni muone kama kuna gofu nairobi, kampala ama addis. kama yapo yanakarabatiwa machache kwa sababu maalumu kama vile ikulu, karimjee, old boma, city hall na kadhalika. sasa huyo mjuaji pengine wala habari hiyo hana kuwa si makuukuu yote yanabomolewa

    ReplyDelete
  10. Mimi nilipata bahati ya kuishi marekani sijaona majengo machakavu katikati ya jiji kila sehemu ni mapya tu. Nilisikitika sana nilipoenda Zanzibar nikaona majengo ya 1800 na kitu bado yapo yanachukua nafasi kubwa ya mji bila ya faida yoyote kwa wananchi kisa eti watalii huu ni upuuzi mtupu.

    ReplyDelete
  11. HAWA JAMAA KWA KULALAMIKA HAWAJAMBO..SEHEM ZA KUMBUKUMBU ZIKO NYINGI SANA ZIMEBAKI NA ZIMETUNZWA, NA ZINAONESHA KUMBUKUMBU YA DAR ES SALAAM SIO SAMORA PEKE YAKE, HAYA MAJENGO HAYAFAI TENA KUISHI WALA KUA KUMBUKUMBU, BASI NA ZILE KOTA ZA POLISI ZA MAGOMENI, CHANG'OMBE NAZO TUACHE KAMA KUMBUKUMBU???

    ACHENI LAWAMA ZISIZO NA MSINGI, KUNA MAENEO MENGINE LAZIMA YABADILISHWE SURA NA MJI KUPENDEZA SIO KILA SEHEM ITAKUA YA HISTORIA TU.

    ReplyDelete
  12. Kwanini wasijenge uswahilini badala ya kucongest city centre? Uswahilini itadevelop lini? Hayo majengo ni ya kihistoria na kamwe hujasikia yanaporomoka kama wanazojenga wao sasahivi ya material kutoka china na wajenzi wa kichina.

    ReplyDelete
  13. HEBU ACHANI UJINGA,TUNATAKA KWENDA NA WAKATI,HAYA MAJENGO NI MAGOFU SASA NI HAKI YABADILISHWE NA MJI UWE WA KISASA.MDAU LONDON.

    ReplyDelete
  14. Wow! Huyo mdau wa nane pole sana ndugu yangu. Majengo ya zamani yanavutia sana watalii. Uingereza majengo yanayobomolewa ni yale yalio jengwa na wabishi na wenye kuifikiri watu hawastahili nafasi kubwa. Lakini majengo mengi ni ya zamani sana na ndio kivutio kikubwa sana cha watalii. Ndio maana yanaitwa 'listed buildings'. Inabidi waingereza wajenge magorfa maana nafasi ni ndogo. However sisi tunanafasi kubwa sana.Kwahiyo maendeleo ni ku expand mji. Sio kubanana na kuharibu historic buildings.

    ReplyDelete
  15. Real tunahitaji skyscapper kwa sasa, no more old building. Waende bagamoyo ma Zanzibar wakaangalie ya kale.

    ReplyDelete
  16. majengo ya zamani kuyagharamia ni gharama sana afadhali yavyunjwe tu.

    ReplyDelete
  17. Jengeni kwanza park za magari dar mji hauna mvuto

    ReplyDelete
  18. Ninahoshangaa mimi ni kuwa sasa hivi Tanzania hakuna utu tena.

    Wale jamaa waliokuwa wanaishi na kufanya biashara hawajapewa hata muda wa kutoa mali zao.

    Wengine kodi ilikuwa haijaisha. Kila mtu anaongelea majengo mapya pasipo kujali binadamu wenzetu.

    ReplyDelete
  19. nakubaliana na wadau wa mwanzo nafikiri wangepanga kupanua mji na sio kuyavunjya haya labda wangeyafanyiaukarabati na kama isingewezekana kukarabati ndipo wafikirie kulivunja , ukweli ni kwamba kuna tajiri kashakula na serikali hii kuna mabilioni ya fedha ambazo zilitakiwa ziwe za raia watu washazipigia hesabu tayari, nyie laleni usingizi , hapa bongo bandugu zangu

    ReplyDelete
  20. Majengo yamekua magofu kwa sababu hayakutunzwa na kitengo husika cha serikali. yaani Antiquities. SDM is an eye sour already

    ReplyDelete
  21. In actual fact it worth preserving history. But lets see what is happening in.bagamoyo. Kilwa zanzibar etc. Preserved buildings are left to delapidate and colapse. Therefore no benefit. Antiquite department need to be enabled. Looking on construction technique and building materials such buildings were tobe destroyed all. And construct new ones alike. Therefore the issue of conservation could work. But most of buildings are ireparrable.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...