Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo, Agosti 29, 2013 baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsindikiza Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo, Agosti 29, 2013 baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini.
Rais wa Burundi, Piere Nkurunzinza, akiagana na baadhi ya maofisa wa Ofisi ya Makamu wa Rais, waliofika uwanjani hapo kumsindikiza leo Agosti 29, baada ya Rais huyo kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini. Kushoto ni Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na viongozi wengine, wakimuaga Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo, Agosti 29, 2013 baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini. Picha na OMR.




nimeipenda hii. inaonyesha kweli Tanzania tumebarikiwa na amani kiasi cha Raisi wa nchi tofauti kuja si kikazi, bali ni mapumziko tu! Mungu ibariki Tanzania. Wote wanaoitakia mabaya na nia ya kuivuruga washindwe!
ReplyDeleteMdau wa Kwanza Wabaya wetu wamesha shindwa vibaya sana!
ReplyDeleteHawana mpya na sasa wanaona aibu na siku zao zinahesabika tunawatambua na tutawatia mkononi na kuwa adhibu vikali.
Mdau wa Kwanza umenena!
ReplyDeleteHalafu,
1.Ndugu zetu baadhi ya Madiaspora Ughaibuni eti ohhh haturudi Tanzania kuna shida!,,,mnaona hao Maraisi wa nchi zingine wanakuja Bongo kupumzika?
2.Na wandugu zetu wengine hapa Tanzania wana panda madege kwenda nje Mapumziko wakati watu na Maraisi wengine wanakuja kupumzika na kustarehe Tanzania?
Katika Maraisi wa nchi Jirani za Afrika Mashariki afadhali huyu Ndugu Pierre Nkurunzinza anaaminika na inaonyesha hana agenda za siri, lakini wengine ohhh !, hala tia maji, tia maji!
ReplyDeleteNdio maana waamtenga jamani wenzake akina UK, M7 na PK !!!
Mapumziko ni pamoja na kubadili mazingira, ndiyo maana watz wanatoka kwenda nje kupumzika na wageni kuja Tz kupumzika. Waswiss wanapokwenda Z'ba haimaanishi kuwa Geneva au Zurich ni pabaya ukilinganisha na Unguja na Pemba. Kama hiyo haitoshi, Uswiss kuna amani kuliko mahali popote duniani, ndiyo maana hawana jeshi. Lakini pia kupumzikia nyumbani kama uwezo haukuruhusu kutoka, siyo mbaya.
ReplyDeleteMdau wa tatu,umejiuliza katumia hela yake au ya walipa kodi? Hakuna haja ya kulinganisha na waenda ulaya,ni uhuru wa mtu kuamua wapi pa kwenda ktk likizo. Mambo ya ushabiki bila uchambuzi hayana mshiko . Kila mtu anasababu zake za kusafiri. Safiri kutoa ujinga na kupanua knowledge. Mimi na ndugu kibao ulaya,hunitumia tiketi kuwaona na kujuana na vichanga vyao,sasa kisa cha kunipiga madongo nini? Bongo ni home tu no matter what!!!
ReplyDeletehuyo mdau mmoja yeye kazi kulaumu watu wanaoishi ughaibuni tu kwani suala la amani mbona obama alikukatazeni hata kwenda mjini na mkapewa likizo ya siku tatu au sio nyie....?
ReplyDeleteMimi mbona nilikuwa Bongo mwezi huu kwa mapumziko kutoka ughaibuni. Lakini, sikupumzika kabisa. Barabara zote zinatengenezwa upya, magari foleni balaa, nilikoswakoswa na bodaboda mara nne katika wiki tatu, niliona accident mbaya mbili za pikipiki na magari. Kwa kifupi, mazingira ya kupumzika hamna Dar Es Salaam kwa sasa. Vitu Tanzania ni ghali kuliku au sawa na ulaya sasa. Kitu kizuri nilichokiona ni kuwa watu wanachapa kazi sana sasa sio kama zamani na kuna majumba mengi ya starehe na maduka ya kila aina na wananchi wengi sana wana uwezo wa kifedha. Nilitumia Euro elfu mbili haraka sana lakini fujo ya mji ilinifanya nisistarehe hata nilipokimbilia Oysterbay Beach, fujo za watu hazijapungua, siku hizi kuna usafiri kila kona ya nchi.
ReplyDeleteKumbe ndio maana tulikuwa tunapata usumbufu wa ving'ora na kufungiwa njia kule Masaki na Ostabei kumbe ndo huyu alikuwa anakaa DABO TRII hotel.
ReplyDeleteNilikuwa nashangaa kila siku mbona ning'ora?
Wasalimie huko.
Hivi kwanini baadhi ya watz wanaokosa viza za mataifa ya magharibi wanakuwa na hasira mbaya sana na wana-diaspora??????
ReplyDeleteHivi wadau mnajua maana ya PK = Pasua Kichwa nimemaliza
ReplyDeleteNa kweli mdau umenipa raha PK - Pasua Kichwa na kweli jamaa pasua kichwa kweli hasikikii la muadhini wala mteka maji kisimani.
ReplyDeletehuyu piere ni mtu wa MUNGU sio pritender,ana hofu ya MUNGU BWANA.
ReplyDeleteMdau wa 5 umeexpleini veli welu. Jiniazi!!
ReplyDeletetofauti ya Obama na ndege zetu angalia ngazi za ndege ...duh
ReplyDeleteWarundi si watu wa fujo na visasi. Ona hata Rais wao alikufa ktk ndege ya Habyalimana lkn kimyaaaa! Pia Pierre anasoma haraka alama za nyakati siyo kama Uhuru Kenyatta amevutwa ktk himaya isiyomuhusu atasoma namba za hao jamaa wakishamfaidi! Kuhusu kashikashi za ujenzi wa barabara yataka uvumulivu tu wa muda kama miaka miwili kisha faida yake wanajiji mtaiona.Mpango wa mabasi ya haraka umefanikiwa sana ktk nchi ya Uturuki(Istanbul) hadi unaona raha licha ya kuwa na watu wengi.
ReplyDelete