Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Usu
Mallya (wa pili kulia) akizungumza na wahariri kutoka vyombo mbalimbali
vya habari. Alioambatana nao ni viongozi anuai, watendaji na baadhi ya
wanachama wa TGNP. katika mkutano na wahabari.
Sehemu ya jopo la viongozi na wanachama wa TGNP wakiorodhesha maswali
ya wahariri (habapo pichani) kabla ya kuanza kuyatolea majibu kwenye
mkutano huo leo.
Baadhi ya wahariri kutoka vyombo vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa katika mkutano na TGNP.
Katika
mkutano huo na wahariri TGNP imeainisha baadhi ya mafanikio na
changamoto ambazo mtandao huo umezipata, ikiwa mbioni kufanya tamasha la
mwaka huu ambalo litafanyika Septemba 3 hadi 6 2013, Katika viwanja vya
TGNP Mabibo.
TGNP
inatarajia kutumia Tamasha la Jinsia kuwapa wanawake fursa ya kushiriki
mijadala ya wazi na kupaaza sauti zao, tamasha hili litashirikisha
wanawake, wanaume, Vijana na watoto zaidi ya 5000 kutoka mikoa yote ya
Tanzania na nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Amerika.
TGNP
imebainisha kuwa kupitia Tamasha hilo, wanawake na wanaume wanaoshiriki
wanapata fursa ya kujijengea uwezo wa kutumia mbinu za kiraghibishi
katika, uchambuzi wa sera , bajeti ya kijinsia, kujadili kwa pamoja na
watendaji wa serikali kuu na za mitaa walioalikwa namna bora ya utoaji
huduma ambazo zitamfikia kila mwananchi.
Pamoja
na mijadala hiyo ya wazi, kutakuwa na mahakama ya wananchi (Popular
tribunal) itakayoendeshwa na Chama cha Majaji Wanawake (TAWJA), watunga
sera, wanasheria, wanaharakati waliobobea kwenye masuala ya Kisheria na
wananchi walioathiriwa na mfumo kandamizi na kukosa msaada wa kisheria
au kuathika na hukumu zilizotolewa.
Aidha
siku inayofuata kutakuwepo na Bunge la wananchi ambalo litaongozwa na
wanazuoni na wataalamu wa sheria na wananchi wote watapata fursa ya
kushiriki kikamilifu.
Mijadala mingine italenga katika masual ya haki ya uchumi kwenye
upatikanaji wa huduma za msingi za jamii kama maji, afya, elimu,
miundombinu na haki ya jamii katika umiliki wa rasilimali ardhi.
Aidha
suala la Katiba mpya litapewa kipaumbele katyika mijadala
itakayopfanyika ikiwepo kuendelea kudai ushiriki ulio sawia katika fursa
na michakato iliyosalia kufikia kupata katiba mpya ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...