Msaidizi wa Makamu wa Rais wa masuala ya Maendeleo ya Jamii, Mgeni Feruzi Kayanda, akimkabidhi Pikipiki Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Geodan Rugimbana, aliyeikabidhi Pikipiki hiyo kwa wananchi wa Mji mpya wa Mabwe pande kwa niaba ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo katika mji huo mpya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mji Mpya wa Mabwe Pande, Abdallah Kunja.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Geodan Rugimbana, akizungumza na wananchi wa Mji mpya wa Mabwe Pande, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Pikipiki kwa wananchi wa mji huo mpya, ambapo Mkuu wa Wilaya, alikabidhi Pikipiki hiyo kwa wananchi wa Mji mpya wa Mabwe pande kwa niaba ya Makamu wa Rais.
Msaidizi wa Makamu wa Rais wa masuala ya Maendeleo ya Jamii, Mgeni Feruzi Kayanda, akizungumza machache wakati wa hafla hiyo baada ya makabidhiano.
Sehemu ya wakazi wa Mji Mpya wa Mabwe Pande waliohudhuria hafla hiyo ya makabidhiano.Picha na OMR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...