Heshima yako Ankal.
Naomba kushea na Wadau swala hili la hali ya mama lishe wa uchina kuhusiana na suala la Usafi.Hapa kwetu Tanzania mama lishe wengi hawazingatii suala la usafi wa Mazingira wanayofanyia kazi.Matokeo yake watu wengi kutopendelea kula/kununua chakula chao.
Hali ni Tofauti China,watu wengi wanakula kwa Mama Lishe kwa sababu mazingira ya maandalizi ya chakula chao ni mazuri.Binafsi walikuwa wananishangaa ninapopata chakula hotelini kwamba ni gharama sana.Yaani Lunch time mtu anabeba familia yake anaenda kupata msosi kwa Mama lishe.Wachina wako busy sana kiasi kwamba hata muda wa kupika wengine hawana!Hapo ni jijini Guangzhou.
Hii ni changamoto kwa mama lishe wa kibongo ambao wametapakaa kila kona.Ni ajira inawaingizia kipato.
Wasukuma Maguta wapo lakini ni wasafi sana,wa kwetu ni wachafu hawaheshimu kazi zao.Niliangalia mambo mengi nikawa najaribu kulinganisha na nyumbani Tanzania.
Wenzetu wako mbali sana.
Na Mdau



Mdau suala la Usafi huko China ni sawa, je ni vipi kuhusu aina ya Vitoweo vinavyoadnaliwa hapo na Mama Lishe wa Kichina?
ReplyDeleteUsije kulishwa supu ya Kenge au Nyoka ukidhani ni Samaki pweza!
Hoja huko China isiishie kwenye usafi tu.
ReplyDeletePana siku moja Kijijini njia ya kwenda Kilwa nilikuwa napita nyumba moja ya mtu ninayemhahamu wa Kabila fulani nikitokea Shambani yule mwenyeji alikuwa pembeni ya ukuta maeandaa chakula na kitoweo fulani hivi aliponiona nakuja akafunika na ungo haraka!
Sasa nilipo karibia nilaona mkia umetokeza kwa nje ya ungo kumbe mwenyewe hakujua kama ungo umefunika sawa sawa au la.
Kwa haraka nilibaini kitoweo kila kilikuwa ni Panya aliyebanikwa!!!
Sasa Mdau na wewe huko China yanaweza yakakukuta hayo kwa hao mama Lishe wa huko!
Hapalinganishiki na Tanzania, Tz tuna unique yetu ya uchafu. Jamani kwa kweli Tz maeneo mengi ni uchafu! Uchafu huu mpaka lini?
ReplyDeleteHilo dustbin linavujisha unjanonjano ni kitu gani. Huo unjano sio mambo yetu yale? kweli china wasafi. Changamoto kubwa ya mamalishe ni mazingira wanayouzia. ugalimoto, mboga moto, vyombo safi lakini benchi linakaribia kuvunjika. pembeni dimbwi. Shida tupu.
ReplyDeleteMdau ungepost video clip badala ya picha ingetoa maelezo na uelewa zaidi
ReplyDeleteHUKO CHINA MIMBA YA MWANAMKE IKITOKA HUWA WANATENGENEZA SUPU YA PILIPILI.
ReplyDelete