Mhe.Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania nchini Marekani na Mexico akiwa katika picha ya pamoja na Mhe.Charles Stith,Balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania,Tanzania House,Washington DC
Mhe.Liberata Mulamula,Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akiwa katika picha pamoja na Mhe. Charles Stith,Balozi wa zamani wa Marekani nchi Tanzania. Kulia ni Bw.Suleiman Saleh,Afisa Ubalozi wa Tanzania Washington DC

Mhe.Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico ametembelewa na aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Charles Stith Ubalozini Tanzania House Washington DC juzi Jumatano Agosti 27,2013. Balozi Stith alifika Ubalozi hapo kusalimiana na Balozi Mulamula na kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake kushika wadhifa wake mpya wa kuiwakilisha Tanzania nchini Marekani.

 Katika mazungumzo yao,Balozi Stith alionyesha dhamira kubwa na utayari wake kushirikiana na Mhe.Balozi Mulamula katika kujenga mashirikiano baina vyuo vikuu vya Marekani na vile vya Tanzania. Balozi Stith alimweleza Balozi Mulamula kwamba anaifahamu vizuri Tanzania na ni nchi ambayo amekuwa na mahusiano mazuri pamoja na watu wake akiwa Balozi na hadi sasa. Kwa msingi huo, Balozi Stith alibainisha umuhimu wa kuweka mkakati mahususi wa kukamilsha azma hiyo na kuahidi kwamba muda wowote kuanzia sasa yupo tayari katika kutekeleza dhamira hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mhe. Mchungaji Charles Stith karibu tena Tanzania!!!

    Kwa kweli Balozi huyu tutamkumbuka sana Tanzania.

    Miongoni kwa mambo makubwa hapa chini niliyo wahi kushuhudia ktk Kipindi chake Ubalozi wa Marekani ulipokuwa Ofisi za muda baada ya kulipuliwa,

    1.Alikiuwa hapendi kuona Watanzania wakikaa juani kutwa ktk misururu ya Foleni Kusubiria kuhojiwa wakiomba Visa, alikuwa akija anasisitiza Maafisa watoe huduma kwa haraka.

    Akaanzisha utaratibu wa Bookings hivyo kuondoa adha na fedheha kwa Watanzania.

    2.Alikuwa anasisitiza kwa Maafisa Ubalozi kuacha tabia mbaya ya kuwanyima watu VIsa bila sababu na vigezo vya kimsingi.

    3.Ktk kipindi chake ndio utaratibu wa kugonga Mihuri kwenye Pasipoti ya kuwanyima watu visa uliachwa.

    Jamaa ni Muungwana sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...