Sehemu ya Vijana wa Vyuo Vikuu walioshiriki Kongamano la kujadili Rasimu ya Katiba Mpya na Rasilimali za nchi yetu.
 Baadhi ya Mafisa wa Mkoa wa Vyuo Vya Elimu ya Juu CCM wakiwa na mgeni rasmi wa Kongamano,Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo,katika ukumbi wa Riverside,Ubungo.
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano wakifuatilia kwa makini hotuba ya Profesa Muhongo alipokuwa akichambua masuala ya gesi na uchumi.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbali mbali nchini wakichukua habari za Kongamano la Kujadili rasimu ya Katiba mpya na rasilimali lililofanyika katika ukumbi wa  Riverside Ubungo, ambalo liliratibiwa na Mkoa wa Vyuo Vya Elimu ya Juu CCM tarehe 5 Agosti 2013. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nasifu juhudi zinazoendelea katika kuwapa watu elimu na kujadili rasimu ya Katiba mpya na rasilimali. Napenda kujua Mkoa wa Vyuo Vya Elimu ya Juu CCM iko chini ya Wizara ya Vyuo Vya Elimu ya juu? Kama ndio sina neno, lakini kama sivyo, napenda nitoe angalizo kwa uelewa wangu hii inaweza ikaleta matengano ikiwa kila chama kitakuwa na vitu vya kufanya hii ina maana hata vyama vingine vinaweza vikawa na kitu kama hiki lakini kwa chama chao. Kwa nini Wizara isiendeshe hili kongamano? Ningependa nijue tu, na msinielewe vinginevyo. Nafurahia sana watu kuelimishwa na kuhusishwa katika jambo kama hili muhimu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...