Mpiganaji Davis Mosha, Edgar D. Mosha, Mayor wa L.A. Deo Temba (Katikati nyuma) na Army Nando
Mpiganaji Davis Mosha akimpa ushauri Army Nando kuwa asahau yaliyopita na aangalie ya mbele na kumweleza kuwa hiyo ilikuwa ni mchezo tu (It was just a game)
Nancy Assenga ( Mama wa Army Nando), Army Nando, na Deo Temba L.A. Mayor
Mayor wa L.A. Deo Temba, Army Nando, Nancy Assenga (Mama na Meneja) na Mkurugenzi mtendaji wa Swahili TV Bwana Alex Kassuwi mara baada ya kumpokea Nando Los Angeles, California.
Juliet Luangisa, Army Nando na Nancy Assenga (Mama na Meneja wa Nando)
Mkurugenzi Mtendaji Swahili TV Bwana Alex Kassuwi, Army Nando, Walter Minja, Deo Temba na Nancy Assenga-Meneja wa Nando wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumpokea Army Nando Marekani.
MPIGANAJI DAVIS MOSHA "THE CEO" BAADA YA KUONANA NA WATANZANIA WAISHIO L.A. AMWANDALIA HAFLA (BASH) NZITO YA HADHI YA KISTAA (CELEB STATUS) ARMY NANDO KATIKA HOTELI GHALI YA YARD HOUSE L.A. MAREKANI.
Mpiganaji "THE CEO" Davis Mosha katika msafara aliwakaribisha pia chakula cha jioni watanzania zaidi ya ishirini katika hoteli ya bei ghali L.A. Yard House ambayo ipo Downton katikati ya Uwanja wa Lakers (Staples Center) na JW Marriott Hoteli.
Army Nando na Nancy Assenga (Mama mzazi na Meneja wake) wakifurahia chakula katika Yard House Hoteli Downtown L.A.
Juliet Luangisa na Walter Minja wakiburudika kwa misosi ya Yard House.
USIKOSE KUANGALIA EXCLUSIVE INTERVIEW NA SWAHILI TV
USIKOSE KUANGALIA INTERVIEW HII ENDELEA KUANGALIA SWAHILI TV www.swahilitv.blogspot.com
bana nyinyi nini bana.Fanyeni fasta mle wengine mkabebe mabox and wengine lindoni .hii ndo state bwana full adabu na maisha.
ReplyDeleteKumbe huyo Nando ni Mmarekani sio Mtanzania??
ReplyDeleteHivi huyu Bw Temba ni mayor kweli au a.k.a tu? Wadau nijuzeni. Bwa Mosha naona unakula bata mpk kuku anaona wivu i hope haupo kwenye list ya yale mambo tunayosifika nayo cku hizi.
ReplyDeleteMichuzi sijajeruhi hisia za mtu maana nawe kwa kubana wakati mwengine km mkoloni vile:-)
Hhahaha umeona enhee,tulipigwa bao kwa kuambiwa kwamba ni mtanzania ili apate kura/sapoti ya kitanzania hatimaye kufikia lengo lake au malengo yao, ama kweli wahenga walisema penye ukweli uongo ujitenga, watanzania mbona rahisi kuwajua hata kwa tabia.Tulikua na mwakilishi wetu kule simtaji alifanikiwa kufika karibu zaidi na ushindi,hatukusikia bati,chupa,fimbo,kiwembe,kisu wala mkia wa taa.
ReplyDeleteJamani ndugu zangu sijui tutaacha lini kuendekeza sifa zisizo na tija. Kulikuwa na haja gani ya kusisitiza kuwa amempeleka katika hoteli ya bei ghali... Nisiweke kwamba namuonea wivu huyo CEO lakini kwa siku kadhaa sasa sijaona la maana analoongelewa zaidi ya uwezo wake wa kutumbua pesa hizo katika viota vya gharama. Naamini kuna mambo ya maana mengi anayoweza kuyatumia kujitangazia umaarufu wa pesa yake zaidi ya anachokifanya. Sio siri hii publicity anayoifanya imenitia kinyaa.
ReplyDeleteMimi huwa sipendi kabisa kuona mwanadada wa kiafrika na minywele bandia. Inakera sana.
ReplyDeletehaters, haters, haters....tafuta chako utumie, usione WIVU wenzako wanapotumia jacho lao!!! wewe unataka habari za shida, shida tuuuuu!!! sisi tunataka habari za RAHA vile vile cause dunia ina SHIDA na RAHA.
ReplyDeleteDavis Mosha
ReplyDeleteHongera!, Imara!, Waaa!
Mwanawane wacheni ma CEO wetu wa Tanzania wapeperushe vema bendera yetu kwa kula bata Unyamwezini!
Naungana na Mdau wa 7 hapo juu:
Sasa mnataka matanuzi wafanye Wanigeria na Waghana peke yao huko Unywamwezini wakati hata sisi Watanzania Wana wa Jakaya wa Kikwete nasi tunajua kuzitafuta na kuzila Fedha?
Hivi huyo kijana Nando ni MTANZANIA kwa mama na baba au kwa mama kama ni mwenzetu ni wa mkoa gani?
ReplyDeletePongezi Davis Mosha!
ReplyDeleteMdau wa 5 naunga na Mdau wa 7 kuwahakikishia Wamarekani na Ubalozi wao hapa Tanzania kuhusu uwezo wetu Watanzania Kifedha.
Hii itasaidia kuwaonyesha Ubalozi wa Marekani hapa Dar Es Salaam wanaotunyimia viza za kwenda Marekani ndugu zetu wengi wanaoomba visa kila uchao ili Wamarekani wajue kuwa Watanzania uwezo wa Kifedha tunao tunapoomba visa mara nyingine wawe wanatoa visa!
Sasa kwa matanuzi hayo ya ndugu yetu Davis Mosha huko kwao Mafisa Ubalozi Unyamwezini inawezekana kabisa wengine Maafisa hawajawahi kuweza kukanyaga wala kula Hoteli hiyo, Ubalozi wakipata taarifa hizo kwa kigezo cha Uwezo wa Kifedha pana Matanzania tanyimwa visa Ubalozi tena?
Hahahahaha, hehehehehe !
ReplyDeleteMdau wa 10 umenivunja mbavu leo, Mjomba Michuzi uipeleke Posting hii Ubalozi wa Marekani Dar Es Salaam ili waone uwezo wetu Watanzania Kifedha tunapokuwa huko kwao Marekani, sio waendelee tena kutunyima visa zao hapa Dar Es Salaa.