Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga(kulia) akibadilishana hati za makubaliano ya mikataba ya ushirikiano na Mwanzilishi wa kikundi cha kimataifa cha Vijana kutoka Korea(IYF) Mchungaji Mwandamizi Ock Soo Park (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Mchungaji Mwandamizi huyo ambae ametia saini kwa niaba ya kikundi cha IYF(International Youth Fellowship) . Hafla hiyo pia ilishuhudiwa na Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara(katikati).
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Dkt, Elisante Ole Gabriel (kulia)akiongea katika hafla ya kutiliana saini mikataba ya ushirikiano leo jijini Dar es Salaam baina ya Wizara yake na Kikundi cha Kimataifa cha Vijana kutoka Korea (IYF).Pichani aliekaa katikati ya bendera ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni naMichezo Mh,Dkt. Fenella Mukangara.( kulia aliokaa) Ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bibi Sihaba Nkinga. (kushoto) Mwanzilishi wa IYF , Mchungaji Mwandamizi Ock Soo Park kutoka kanisa la Good News Gangnam. Seoul Korea.
Baadhi ya vijana wa kikundi cha IYF kutoka korea wakiohudhuria katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo.Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akipokea Tuzo kutoka kwa Mwanzilishi wa IYF ya Korea Ock Soo Park , ambae pia ni Mchungaji Mwandamizi wa Kanisa laGood News Gangnam.Dhumuni ya tuzo hiyo ni kwaajili yakumpongeza Mh,Waziri huyo kwa jitihada za kazi zake .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...