Leo, waMarekani wameadhimisha miaka 50 tangu kufanyika kwa maandamano makubwa ya kudai haki za watu weusi. Katika maadhimisho hayo, kamera ya swahilivilla blog iliegeshwa kando ya mlango wa kuingila na kushuhudia watu maarufu hapa nchini wakipekuliwa kwa sababu za usalama kabla ya kuingia ndani sherehe hizo ambazo ambazo zimehudhuriwa na maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali nchini hapa.
Tuliobahatika kuwanasa katika kamera hiyo ni pamoja na muigizaji Jamie Foxx, pale alipotolewa ndani ya gari na maofisa kuanza kupekua gari alilolipanda kabla ya kuingia ndani ya eneo la Lincoln Memorial  Washington DC. 
Mwigizaji wa filamu Angelha Bassett Evelyn alipotolewa kwenye gari lake na  maofisa kuanza kulipekua kabla ya kuingia ndani ya eneo la Lincoln Memorial  Washington DC
Mshangao mkubwa watu walioupata ni pale mtoto wa Rais wa zamani nchini Marekani John F. Kennedy, Caroline Kennedy ambae ni balozi mteule Nchini Japani, alipoingia na Cab (Taxi). cha kuchangaza pia ni pale gari lake lilipopekuliwa bila ya kujali ukubwa au cheo alichonacho na kufata sheria ya upekuzi kama wengine magari yao yalivyopekuliwa.
Muigizaji maarufu wa filamu nchini Marekani Forest Whitekar nae pia gari lake lilifanyiwa upekuzi na maofisa wa usalama baada ya kuwasili katika endeo la Sherehe za miaka 50 ya March on Washington DC
Vile vile kamera ya swahilivilla blog imemnasa Rajiv “Raj” Shah American Economic development specialist, alipotolewa nje ya gari lake na kufanyiwa upekuzi wa lazima siku ya Jumatano Aug 28, 2013 Washington DC
Watu tupo kazini..: Ofisa Usalama akifanya upekuzi wa magari ya watu maarufu yanayoelekea katika maadhimisho ya miaka 50 ya March on Washington DC siku ya jumatano Aug 28.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hapa watu tupo kazini utatuambia nini? sio nyinyi huko kwenu Africa kuendekeza udikteta, et mzee weee pita ni kiongozi mkuu. Sio hapa, watu na proffesion zetu chezea sisi, una than hii third word ya kunyanysana, hasa kwa wasio na kitu, chezea sisi, hatunyanyasani hapa. wote ni sawa tu, hakuna cha kigogo, wala mkubwa wa serikali wala nini? wote ni sawa tu, kila mmja na madaraka yake yake ya kazi na wajibu wake.

    ReplyDelete
  2. USA wanajifanya wako mbele. Askari hata uniform hawavai!!

    ReplyDelete
  3. Eti huko kwenu Africa,halafu ndio mnataka uraia wa nchi 2 huku mnatudhihaki,nyi endeleeni kuchambisha wazee huko na sisi mtuachie Africa yetu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...