Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi ambae pia ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM wa Mikoa,Ally Mohamedi Mtopa |
Kikundi cha ngoma cha Kiwalala kikitumbuiza katika maonyesho hayo
Jengo la Maonesho ya Nane Nane
Kutoka kushoto....Waziri wa Tamisemi, Mhe HawGhasia Mwenyekiti wa Taso kanda ya kusini,Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Mathias Chikawe (Mgeni Rasmi) Mkuu wa mkoa wa Lindi na Mkuu wa wilaya ya Lindi
Wakuu wa wilaya za mkoa wa Lindi na Mtwara
Washindi wa jumla maonesho ya nane nane wakisherehekea
-------------------
Na Abdulaziz Video
SERIKALI imetakiwa kutekeleza agizo lililotolewa na Chama cha
mapinduzi (CCM) la kuwalipa fedha zilizobaki wakulima wa korosho kanda
ya kusini,inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara,ili kuondoa
malalamiko yasiyo ya msingi zidi ya Serikali yao.
Akitoa salamu za CCM,Mwenyekiti wa Mkoa ambae pia ni Mwenyekiti wa
Wenyeviti wa CCM wa Mikoa,Ally Mohamedi wakati wa ufungaji wa maonesho
ya 4 ya wakulima nanenane,kanda ya kusini yaliyofanyika viwanja vya
ngongo katika Manispaa ya Lindi,alisema anashangazwa kuona Serikali
ikishikwa na kigugumizi katika kutekeleza agizo iliyopewa Na Chama
chake kuingilia kati mgogoro wa wakulima wa korosho,ikiwemo kuwalipa
fedha zao zilizosalia baada ya zao hilo kukosa soko.
“Chama kilishatoa agizo kwa kuitaka Serikali kuingilia kati ikiwa ni
pamoja na kuwalipa wakulima wa korosho fedha zao zilizobakia Baada ya
pilikapilika na kupiga kelele juu ya masuala ya korosho,Chama
kilinituma nikaonane na waziri mkuu,kumuulizia lile agizo April 23
mwaka huu,la kuwalipa wakulima wa korosho Sh,600/-limefikia
wapi?,,,,,,lakini kwa bahati mbaya sikupata nafasi ya kuonana nae
kutokana na kuwa katika ziara za kiserikali sasa serikali ipo hapa
nyie mawaziri ndio serikali mnamuogopa nani?”Alisema Mtopa.
Akasema kitendo cha Serikali kuendelea kulifumbia macho agizo
lililotolewa na Chama chake,juu ya malalamiko ya wananchi,
kinawanyong’onyesha na kuwakatisha tama wakulima wakiwemo wa korosho.
Pia,mwenyekiti huyo wa Chama mkoani Lindi,alisema inakuwaje Bodi ya
korosho au vyama vya msingi vya ushirika wa ununuzi wa mazao vinakuwa
na nguvu kuishinda Serikali katika kutatua kero za wananchi wake.
Mtopa amesisitiza kwa kutoa angalizo,iwapo Serikali hawatalipa fedha
kwa wakulima hao wa korosho,kuna hatari ya wananchi kutoendelea
kukiamini tena Chama hicho katika chaguzi zijazo ikiwemo katika
utekelezaji wa Stakabadhi ghalani.
Naye,waziri wa katiba na Sheria,Mathias Chikawe,ambaye alikuwa ni
mgeni rasmi katika ufungaji wa maonesho hayo ya nanenane,amehaidi
kukutana na mawaziri wenzake kwa lengo kuyazungumza,kabla ya kukutana
na waziri mkuu.
"Naahidi kulifanyia kazi pamoja na mawaziri wenzangu hata hivyo
tutapiga debe pia ili Nane nane mwakani Kitaifa iwe Viwanja vya Ngongo
kwa mara ya kwanza kanda ya kusini
Mwanzoni mwa mwaka huu,wakulima wa korosho wilaya tatu kati ya tano za
mkoa wa Lindi, ambazo ni Liwale, Ruangwa na Kilwa,walifanya vurugu
ikiwemo kuharibu mali za viongozi wakiwemo wanasiasa na vyama vya
msingi vya ushirika.
Huyu Waziri jina la baba ni Ghasia sio Gasia kama wanavyotamka wasomaji wa habari maredioni na ma-tv-ini. Ghasia ni neno la Kiswahili ambalo maana yake ni kelele. Gasia sio neno la Kiswahili.
ReplyDelete