Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imejadili na kutolea maamuzi pamoja na mambo mengine suala la Madiwani wanane waliotangazwa kufukuzwa uanachama na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera.

Katika maamuzi yake, Kamati Kuu imebatilisha uamuzi uliofanywa na Halmashauri Kuu CCM ya Mkoa wa Kagera Agosti 13, 2013 wa kuwafukuza uanachama Madiwani hao. Hivyo Madiwani hao wanane ni wanachama halali wa CCM.

Kamati Kuu imetoa uamuzi huo, baada ya kubaini kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera haikuzingatia Katiba ya CCM ya 1977 Toleo la 2012 Ibara ya 93 (15). Ibara hiyo inasomeka kuwa moja ya kazi ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ni:-
“Kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, isipokuwa kwa suala la kumvua uanachama au uongozi Diwani lisifanyike hadi Kamati Kuu imearifiwa na kutoa maelekezo”.

Aidha, Kamati Kuu imewaonya Madiwani wa CCM wa Manispaa ya Bukoba, Mbunge wa Bukoba Mjini na Meya kwa kusababisha kukosekana kwa utulivu, mshikamano na amani katika Manispaa na Chama.

Kamati Kuu pia imeitaka Serikali kumwagiza mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali(CAG) kufanya ukaguzi maalum wa haraka wa mambo yanayolalamikiwa dhidi ya Meya ili ukweli ujulikane na matokeo ya uchunguzi huo yasilishwe kwenye baraza la madiwani ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazoongoza Serikali za Mitaa.

Wakati tuhuma hizo dhidi ya Meya zikichunguzwa; Kamati Kuu inawataka Madiwani wa CCM  kurejesha utulivu kwenye Manispaa na Chama kwa ujumla ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi wa Bukoba.

Imetolewa na:-

Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM
ITIKADI NA UENEZI
27/08/2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kaka safii kabisaaaa hili jamaaa limea limefanya madudu sana na Mkuu wa mkoa na yeye nintatazo sanaa Muheshimiwa Rahisi alipo kuwa hapa alimsinamamisha mkuu wa mkowa akajibu mambo yote tutayatekeleza na kuhusu harusi na muda utaongezwa lakini juzi tu afisa utamaduni ameulizwa akasema mkuu wa mkoa amekataa. sasa siunaona alivyo na dhalau.

    ReplyDelete
  2. Huyu mganda wange limuondoa tu alisha vuluga chama akiwa mwenyekit cafu ikachukua na mbaya zaid mpaka wakaita zanzba ya bara bk, kagasheki alipokuja kwa nguvu zote akakomboa jibo na akaaid kuifuta kabisa caf na kweli akaifuta sasa huyu jamaa kaludia yaleyale, siyo mzalendo kabisa, kwanza yeye si mea mwambie atembee kwa miguu kama hajapigwa mawe na wananchi wenye hasira kali.

    ReplyDelete
  3. Kwa Muheshimiwa Rais. Alipo kuja bkb, mbuge wetu alimwambia mambo 3 muheshimiwa Rais 2akatoma majibu kupitia kwa Magufuli na Mwakiembe 1 kuhusu muda wa Mahurusi kuongezwa akamuita mkuu wa mkoa nae mbele ya Rais wetu akaid kulifanyia kazi tena hata redio zilikuwa hewani na watu wakashangilia, na kufurahi kweli sasa alipoulizwa afisa utamaduni akajibu mkuu wa mkoa amekataa anasema yeye ndo rahisi wa mkoa kweli! na sisi niwatanzania nahii ni nchi yetu soten na sisi siyo wafungwa, muheshimiwa Rais ni mtu wa watu na anapenda wanachi wakesanaaa ila hawa viongozi ndo wanao halibu, mwisho Muheshimiwa Rais tunakuomba umuulize mkuu wa mkowa huu ubabe anautoa wapi? je na wewe ungekuwa na ubabe kama huu sisi wanyonge tungelioshi kweli!. michuzi tafadhali ni positie hii comment na hakuna nilicho zusha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...