Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dares salaam juu ya hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Uchukuzi juu ya sakata la madawa ya kulevya yaliyokamatwa huko Afrika Kusini hivi karibuni.Dkt. Mwakyembe amewafukuza kazi mtandao mzima uliohusika kusaidia kusafirisha madawa hayo, pia Waziri Mwakyembe ameliagiza jeshi la Polisi kuwakamata wafanyakazi hao na kuwaunganisha na wenzao kujibu mashitaka ya jinai.
Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akionyesha picha ya Msanii Agness Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa habari,masogange alikamatwa na madawa ya kulevya huko nchini Afrika Kusini hivi karibuni.
waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Uchukuzi akiwa anafafanua hatua zilizochukuliwa na Serikali kuushughulikia mtandao mzima uliosaidia kupitisha madawa ya kulevya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. This is very strange, Polisi wenye kazi yao wako kimya na waziri anayetakiwa kushughulikia miundombinu ya uchukuzi sasa hivi anashughulikia madawa ya kulevya...Kuna nini hapo jamani???

    ReplyDelete
  2. Hongera sana waziri Mwakyembe. Ikomboe Tz kutokana na hayo majanga mana sasa mambo ya kusafiri nje ya nchi mtu anapekuliwa na kuogwa x-ray hata zisizo na uhitaji wakati hizo x-ray zaina amdhara mwilini sasa upigwe bila sababu ya kiafya inakuwa sio vizuri. Mungu endelea kumtumia waziri Mwakyembe mpaka biashara ya madawa ya kulevya itokomezwe kabisa Tz. Yani nimefurahi sana sana mana sasa angalau wasafiri tusiofanya hizo biashara tutakuwa na amani. Mwakyembe juu juu juu zaidi.

    ReplyDelete
  3. Hongera sn sasa polisi walikua wanahunyahunya nn, hii wizara ya mambo ya ndani ingevunjwa maana kama imeshindwa kazi,naitwa mdudu KAKAKUONA mwenye macho ma3,

    ReplyDelete
  4. Tunaomba waziri Mwakyembe aungwe mkono na serikali.Pia kaka michuzi huo mtandao mzima ni kina nani?tupatie majina kama Mheshiwa aliwataja.

    ReplyDelete
  5. Tanzania tungepata viongozi wa ukweli kama mr mwakyemba nchi yetu ingeendelea vizuli fanya kazi baba mungu hatakulinda kamata wote wausikia fungilia mbali

    ReplyDelete
  6. Sasa kwenze swala hili mbona waziri husika (Nchimbi) hatumsikii??

    ReplyDelete
  7. Hao watu ambao mwakyembe amependekeza wakamatwe hta wakikamatwa najua Polisi watasema hawana Ushahidi hapo ndio mwisho polisi bongo tatizo kubwa na hata wakiwakamata hawatawafungulia mashtaka na hata wakiwafungulia mashtaka serikali haitashinda kesi hata kama ushahidi upo!!!!!



    ReplyDelete
  8. Mdau wa kwanza kwa hiyo unataka hii biashara iendelee!!! hivi unaelewa mana ya uchukuzi au usafirishaji?Mbona hivyo jamani. Au nyie ndio mnataka kuvuliwa nguo kwenye airport za watu nje?Je umewahi kusafiri mara kwa mara nchi za wenzetu? basi naomba ukae kimyaaa mwache Dr. mwakyembe afanye kazi yake, kama una undugu na Agnes imekula kwako! Dr. Mwakyembe juu juu juu zaidi, hakuna wa kulinganishwa naye jamani.

    ReplyDelete
  9. Mdau unayetaka kumsikia Nchimbi hata sikuelewi, kazi ni kazi! Je nchimbi ni wa uchukuzi naye? Ila ukipenda mtafute uongee naye ili umsikie. Watanzania hivi tutaendelela lini?

    ReplyDelete
  10. Isiishie kushusha rungu kwa wasafirishaji na maofisa wa uwanja wa ndege pekee,zoezi liende mbali zaidi hadi kwa wamiliki wa dawa hizo wanaowatuma wasaii njaa kuzisafirisha na hapo ndo tutaondokana na aibu hii.

    ReplyDelete
  11. Muacheni Nchimbi na polisi wake wako busy na Sheikh Ponda na matumizi yalioshamiri ya tindikali

    ReplyDelete
  12. Jamani wadau naomba namba ya simu ya mweshimiwa waziri Mwakyembe. ili tusaidiane kazi hii.
    Mckenzie

    ReplyDelete
  13. Beautiful, I love this guy.

    ReplyDelete
  14. acha ufinyu wa fikra we mchangiaji wa chini hapa, hili ni swala mtambuka(cross cutting issue) kila mtu ana sehemu ya kulifanyia kazi hadi house girl wako. sasa unashangaa nini waziry mwenye dhamana ya usafirishaji ambaye reputation ya uwanja wetu wa ndege mkuubwa ikibomolewa inakula kwenye ufanisi wake?

    anza kuviangalia vitu kwa jicho la ndege sio kama panya buku...

    ReplyDelete
  15. Kweli Mwakiembe ni Kiongozi tuliyepewa na Mungu. Na Hafi ila kwa ridhaa ya Mungu. Songa Mbele Mwakiembe; Mungu yupo nawe, Tunakuombea

    ReplyDelete
  16. Hongera sana Mh Mwakyembe. Mungu anendelee kukupigania. Tunahitaji viongozi kumi kama wewe na Tanzania itanyooka.
    Shughulikia pia na swala la uwizi wa mizigo airport na swissport. Tumechoka kuibiwa. Hili tatizo ni sugu na la mda mrefu sana.
    Ukienda kulalamika hamna msaada wowote na ushahidi wamepoteza

    ReplyDelete
  17. Donnydoc usAugust 17, 2013

    Hong era sana Mh.Mwakyembe kwa kazi Nouri

    ReplyDelete
  18. Mawaziri wengine wapigwe short course na mwakyembe jinsi ya ku run wizara zao,msimamiaji WA course hiyo awe meakyembe.this man is great he should be the prime minister.

    ReplyDelete
  19. Mwakyembe chondechonde ukimaliza huko hamia kwa walioshafirisha/wanaosafirisha wanyama KIA.Maaana nao wanakuharibia wizara yako.Pamoja na madawa yanayopitia KIA pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...