Kwa mara ya kwanza Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR-MUU)
imeendesha mkutano wa kikazi kwa njia ya Kielektroniki
(e-Conference).Mkutano huo uliofanyika leo kwa muda wa saa tano umefanyika
kwa kuziunganisha OR-MUU na Ofisi za Katibu Tawala wa Mikoa ya
Kilimanjaro,Kagera na Iringa.
Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.Hab Mkwizu (wa pili kulia) akiwakaribisha washiriki kutoka Kilimanjaro,Kagera na Iringa katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya elektroniki (e-conference) mapema leo.
:Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Faisal Issa akiuliza swali wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya elektroniki (e-conference) iliyounganisha ofisi za Katibu Tawala Mkoa wa Kagera,Iringa na Ofisi ya Rais,Utumishi mapema leo.
Walikuwa wanasubiri nini kuanza kutumia technology hiyo?
ReplyDeleteafadhali...heko na mwendo mdundo...
ReplyDeleteSWALI NI MOJA, JE HAYO MAWASILIANO YAPO SECURED??? MAANA INAWEZEKANA VIKAO MUHIMU VYA NCHI VIKAWA VINAFANYIKA NA IKAWA RAHISI KUINGILIWA KATI EIDHA NA WATU BINAFSI, NCHI JIRANI, NK NA ZIKAVUJA NJE.
ReplyDeleteNI VYEMA KWA SERIKALI NA WAHUSIKA KULIANGALIA ILI SWALA ILI TUPATE UHAKIKA NA KULINDA SIRI ZA SERIKALI NA NCHI YETU KULIKO KWENDA TU SABABU TENDA IMETOLEWA NA KAZI IMEFANYIKA!!
Safari za nje kwa ajili ya makongamano, semina, warsha, ziara za mafunzo, kubadilishana uzoefu,kuanzisha miji-dada n.k ambazo zilifanya wafanyakazi wa serikali kuu na serikali za mitaa kumungunya bajeti ya walipata kodi sasa natumai zitapungua au kuisha kabisa.
ReplyDeleteMdau
Mlipa-Kodi
Heko!!!
ReplyDeleteHii itapunguza gharama za utitiri wa Vikao na Safari za Mikutano isiyokwisha.
Kwa heri Bahasha za Khaki kwenye Vikao vya Kiserikali!!!
ReplyDeleteDuhhh !
ReplyDeleteMwaka wa njaa kwa sisi Maafisa wa Serikali umeingia.
Huu ndio mwisho wa kuongeza masifuri katika Risiti za gharama za Safari za Kikazi kuhudhuria Mikutano, ili baada ya kurejea Kituo cha kazi tunawasilisha madai.
Ohhh sijui nyumba yangu iliyoishia kwenye Renta nitamaliza vipi?