Kwa mara ya kwanza Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR-MUU) imeendesha mkutano wa kikazi kwa njia ya Kielektroniki (e-Conference).Mkutano huo uliofanyika leo kwa muda wa saa tano umefanyika kwa kuziunganisha OR-MUU na Ofisi za Katibu Tawala wa Mikoa ya Kilimanjaro,Kagera na Iringa.
Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.Hab Mkwizu (wa pili kulia) akiwakaribisha washiriki kutoka Kilimanjaro,Kagera na Iringa katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya elektroniki (e-conference) mapema leo.
:Katibu Tawala wa Mkoa wa  Kilimanjaro Dkt.Faisal Issa akiuliza swali wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya elektroniki (e-conference) iliyounganisha ofisi za Katibu Tawala Mkoa wa Kagera,Iringa na Ofisi ya Rais,Utumishi mapema leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Walikuwa wanasubiri nini kuanza kutumia technology hiyo?

    ReplyDelete
  2. afadhali...heko na mwendo mdundo...

    ReplyDelete
  3. SWALI NI MOJA, JE HAYO MAWASILIANO YAPO SECURED??? MAANA INAWEZEKANA VIKAO MUHIMU VYA NCHI VIKAWA VINAFANYIKA NA IKAWA RAHISI KUINGILIWA KATI EIDHA NA WATU BINAFSI, NCHI JIRANI, NK NA ZIKAVUJA NJE.

    NI VYEMA KWA SERIKALI NA WAHUSIKA KULIANGALIA ILI SWALA ILI TUPATE UHAKIKA NA KULINDA SIRI ZA SERIKALI NA NCHI YETU KULIKO KWENDA TU SABABU TENDA IMETOLEWA NA KAZI IMEFANYIKA!!

    ReplyDelete
  4. Safari za nje kwa ajili ya makongamano, semina, warsha, ziara za mafunzo, kubadilishana uzoefu,kuanzisha miji-dada n.k ambazo zilifanya wafanyakazi wa serikali kuu na serikali za mitaa kumungunya bajeti ya walipata kodi sasa natumai zitapungua au kuisha kabisa.

    Mdau
    Mlipa-Kodi

    ReplyDelete
  5. Heko!!!

    Hii itapunguza gharama za utitiri wa Vikao na Safari za Mikutano isiyokwisha.

    ReplyDelete
  6. Kwa heri Bahasha za Khaki kwenye Vikao vya Kiserikali!!!

    ReplyDelete
  7. Duhhh !

    Mwaka wa njaa kwa sisi Maafisa wa Serikali umeingia.

    Huu ndio mwisho wa kuongeza masifuri katika Risiti za gharama za Safari za Kikazi kuhudhuria Mikutano, ili baada ya kurejea Kituo cha kazi tunawasilisha madai.

    Ohhh sijui nyumba yangu iliyoishia kwenye Renta nitamaliza vipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...