Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Morrice Oyuko kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ukuaji halisi wa pato la taifa kwa robo ya kwanza ya mwaka (Januari – Machi 2013) ambapo uchumi umekuwa kwa kasi ya asilimia 7.5 ukilinganishwa na kasi ya asilimia 7.4 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2012. Ukuaji wa shughuli za uchumi za kilimo zimekuwa kwa asilimia 1.4 ambapo shughuli za uchimbaji madini na kokoto zimeshuka kwa asilimia 4.7 ukilinganisha kwa kasi ya ukuaji wa asilimia 23.8 kwa mwaka 2012.
Baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Morrice Oyuko wakati akiongea nao kuhusu ukuaji halisi wa pato la taifa kwa robo ya kwanza ya mwaka (Januari – Machi 2013) ambapo uchumi umekuwa kwa kasi ya asilimia 7.5 ukilinganishwa na kasi ya asilimia 7.4 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2013. Mkutano huo wa waandishi wa habari umefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa NBS uliopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Morrice Oyuko (hayupo pichani) wakati akiongea nao kuhusu kukua kwa pato la taifa kwa robo ya kwanza ya mwaka (Januari – Machi 2013) ambapo uchumi umekuwa kwa kasi ya asilimia 7.5 ukilinganishwa na kasi ya asilimia 7.4 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2013.Ukuaji wa shughuli za uchumi za kilimo zimekuwa kwa asilimia 1.4 ambapo shughuli za uchimbaji madini na kokoto zimeshuka kwa asilimia 4.7 ukilinganisha kwa kasi ya ukuaji wa asilimia 23.8 kwa mwaka 2012.Picha na Anna Nkinda - Maelezo
MTAZAMO WANGU JUU YA MUUNGANO.
ReplyDeleteKwanza ningeomba tume ya Warioba kuwaelezea wananchi mambo yafuatayo
1. Ni nini faida za muungano.
2. Ni nini hasara za muungano.
3. Ni kwa nini tuliungana.
Baada ya hayo majibu wananchi wayaangalie kwa kina, wanchi wengi hawajui au hawaelewi juu ya muungano leo unawaambia wachangie maoni, wachangie nini?