Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Timu
ya Jeshi la Polisi itakayoshiriki michezo ya Shirikisho la Wakuu wa
Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO Games) inatarajiwa kuondoka Jumanne
Agosti 13 mwaka huu kuelekea katika jiji la Windhock nchini Namibia kwa
ajili ya michezo hiyo.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Afisa Michezo wa Jeshi la Polisi Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi Jonas Mahanga alisema timu hiyo itaondoka na
wanamichezo 67 ambao wanaunda timu za Mpira wa miguu wanaume, Mpira wa
pete Wanawake, Riadha wanaumwe na wanawake na mchezo wa Vishale (Dats).
Mahanga
alisema timu hiyo inaendelea na mazoezi katika kambi yao ya maandalizi
iliyopo katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) ambapo
mpaka hivi sasa wameshacheza michezo kadhaa ya kujipima nguvu na
kufanikiwa kufanya vizuri.
Alisema
michezo hiyo itashirikisha Nchi kumi na nne (14) katika michezo
mbalimbali na lengo la michezo hiyo ni kujenga ushirikiano wa Majeshi ya
Polisi kwa nchi wanachama wa SARPCCO katika kukabiliana na uhalifu.
“Michezo
hii pamoja na kuweka vyema kiafya miili ya Askari wetu, lakini pia
itakuwa ni fursa kwa Askari wetu kufahamiana na wenzao na kubadilishana
uzoefu katika kukabiliana na uhalifu hasa unaovuka mipaka”Alisema
Mahanga.
Mara
ya mwisho Tanzania kushiriki katika michezo hiyo ilikuwa mwaka 2009
nchini Malawi ambapo timu hiyo ilinyakua ushindi wa pili kiujumla .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...