Na Frank Geofay wa Jeshi la Polisi,
Windhoek Namibia.
Timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) nchini Namibia imelazimishwa sare ya mabao 2 kwa 2 katika mwendelezo wa michezo hiyo.
Mchezo huo ambao ulichezwa katika uwanja wa Sam Njoma nje kidogo ya jiji la Windhoek ulikuwa mkali huku Tanzania ikitawala katika vipindi vyote lakini ikishindwa kutumia vizuri nafasi walizozipata.
Mabao ya Kongo yalifungwa katika kipindi cha kwanza na Makundi Kaluma na Kalumba Banza na ya Tanzania yalifungwa na Ahmed Bello kipindi cha kwanza na John Kanakamfumu kipindi cha pili kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa kongo kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Huu ni mchezo wa pili kwa timu ya mpira wa miguu ya Polisi Tanzania kucheza baada ya mchezo wa kwanza kukubali kichapo cha mabao 2 kwa 1 kutoka kwa Zambia.
Katika Mpira wa pete timu ya Polisi Tanzania iliweza kuifunga Angola 61 kwa 13.huku ikitoka sare na wenyeji Namibia kwa kufungana mabao 29 kwa 29 huku ikifungwa na Swaziland 35 kwa 25.
Matokeo mengine katika mpira wa miguu ni pamoja na Zambia 2 Lesotho 0, Namibia 1 South Afrika 0.
Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania itashuka dimbani tena kesho kupambana na Angola ambapo pia wanariadha wanne wataiwakilisha Tanzania katika mbio fupi za kilometa 25.
Mshambuliaji
wa Polisi Tanzania Adimini Bantu (mwenye mpira) akiwatoka mabeki wa timu ya
Polisi Kongo wakati wa mchezo wao katika Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi
kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO
nchini Namibia.Timu hizo zilitoka sare ya 2 kwa 2.
Mshambuliaji
wa Polisi Tanzania Ahmed Bello (jezi ya bluu) akipambana na mchezaji wa timu ya Polisi Kongo wakati wa mchezo wao
katika Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO nchini Namibia.Timu hizo zilitoka
sare ya 2 kwa 2.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...