Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Adam H. Mayingu (pichani) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam jana, Jumanne, Agosti 13, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi unaanzia Juni 8, mwaka huu, 2013.

Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mayingu alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa PSPF.

Bwana Mayingu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga ambaye amestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

14 Agosti, 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...