Mkuu wa wilaya ya Kilwa,Abadalah Ulega akipata maelezo ya ujenzi wa Mkuza wa bomba la gesi kutoka Mtwara kuelekea Dar es Salaam toka kwa Eng Ahmeid Chinemba,Mratibu wa Mradi Mkoa wa Lindi alipokagua kazi zinavyoendelea.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa,Abdalah Ulega akisikiliza maelezo toka kwa Mratibu wa mradi huo,Eng Ahmeid Chinemba alipokuwa akikagua kazi zinavyoendelea za kuandaa njia ya litakapopita Bomba la gesi kuanzia vijiji vya somanga hadi Kiranjeranje wilayani Kilwa.
Kambi ya Njia nne wilayani Kilwa ni Moja kati ya kambi za Wachina Watakaoanza kutandaza bomba la kusafirisha Gesi kati ya Songosongo,Mtwara kuelekea Dar Zikiwa katika hatua ya umaliziaji wa majengo ya kuishi wafanyakazi..Kambi kama hii ipo katika kijiji cha Nangurukuru na Kitomanga wilayani Lindi.

Na Abdulaziz Video,Kilwa

Mkuu wa wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi,Abdallah Ulega amefanya ziara ya siku moja kukagua maendeleo ya Ujenzi wa njia ya bomba la gesi(Mkuza)kazi ambayo imeanza kati ya Songosongo,Mtwara Dar na kutarajiwa kazi zote kukamilika ndani ya Miezi 18.

Ulega alitembelea kati ya kijiji cha Somanga na Kiranjeranje kukagua kazi inavyoendelea na changamoto za na kuzungumza na wananchi na kuwataka waitumie vyema fursa hiyo katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa Ushirikiano kwa wawekezaji ili wanufaike na huduma za kimaendeleo katika wilaya yetu.

“Ndg zangu wana kilwa hizi fursa mzitumie kwa kusomesha watoto wenu ili wanufaike na ajira za gesi hii,Hata hivyo nasikitika kwa kuwa nimeambiwa na hawa wachina kuwa mmeanza kuwaibia jamani tutafika mlikuwa kwa amani na hawa wageni mnapata ajira za muda mnalipwa sasa angalieni tumewaletea askari nyie wenyewe mnaona raha?Serikali imejipanga na kusimamia mnanufaika na miradi hii…alimalizia Ulega alipokuwa akisalimiana na wananchi wa njia nne wilayani Kilwa.

Kwa Upande wake mratibu wa Mradi huo wa Mkuza Mkoa wa Lindi,Eng Ahmeid Chinemba akitoa maelezo ya kazi hizo kwa Mkuu wa wilaya huyo,Alibainisha kuwa kazi hiyo ambayo Itagharimu Jumla ya Dola Bilion 1.2 inatekelezwa na kampuni ya mabomba ya petrol ya China imeanza kwa kuandaa mkuza kati ya Songosongo Nyamwage kuelekea Dar es salaam na Somanga Nangurukuru Mtwara.

Chinemba pia alieleza kuwa sambamba na ukamilishaji wa mkuza huo pia tayari kambi kuu 3 za za malazi na ofisi kwa wafanyakazi wa kazi hizo zipo katika hatua ya mwisho katika Vijiji vya Njianne,Nangurukuru na Kitomanga ambapo pia mabomba ya kazi yakiwa yanapokelewa katika kambi ya Kiranjeranje.

Kufuatia Uwepo wa Gesi asilia ya Songosongo wilayani Kilwa na kusafirishwa kwenda Dar tayari inauzwa kwa zaidi ya Viwanda 30,huku jamii ya wakazi kijiji cha Songosongo wakinufaika na utumiaji wa nishati ya umeme bila malipo huku Halmashauri ya wilaya Kilwa ikikusanya kodi ya Huduma pamoja kusaidia huduma mbalimbali za kijamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Uncle naomba uniulozie kwa viongozi wetu inakuaje miradi ya kichina inaajiri wachina kibao kwa hata zile kazi zinazoweza lufanywa na watanzania miradi kama hii si ndio fursa ya watz kukuza kipato chao ?

    ReplyDelete
  2. Jibu la mdau hapo juu:Kawaida wachina ndivyo wafanyavyo ktk makubaliano yao na hilo halina ujanja kwa viongozi wetu wa afrika nzima si tu tanzania.Kwa sasa china imejaa watu wasio na ajira na seriakli yao inajitahidi kuwapa nafasi nyingi za nje ili wachina watoke nchini na kwenda kufanya kazi nje ya china,matokeo yake ndio hayo tunayoyaona sasa hapa nyumbani.Uhalisia ni kwamba mpaka afrika magharibi kilio ni hikohiko, wanakaba sehemu zote mpaka ufagizi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...