Mhe.  Michael Chilufya Sata, Rais wa Zambia ameonesha kukwerwa Na Unene wa askari Polisi wa Jeshi la Zambia na kuhoji kama kweli ni wakakamavu (Physical Fitness). Aidha, amemwagiza Bibi Stella Libongani, Inspekta Jenerali wa Jeshi hilo kuhakikisha kuwa kuna ukakamavu katika jeshi hilo. Mhe Rais Sata aliyasema hayo katika Ikulu ya nchi hiyo alipokuwa anamwapisha Kamishna Malcolm Mulenga kuwa Mkuu wa Polisi wa Jimbo ya Luapula, nchini Zambia. Kazi kwa Jeshi  Letu la Tanzania.
 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Pamoja na kumpongeza Mheshimiwa Rais Satta kwa maoni yake ya uwazi na ukweli kwa mjeshi wake lakini pongezi nyingine zangu apokee kwa kuwa na simple office!

    Hebu onena Baba wa watu asivyo na makuu! Ka ofisi kake very simple na maji yake ya kunywa mezani I really like this spirit Mr. African President!
    Please keep it up.....

    ReplyDelete
  2. Hahaaaa,JK atangaze hilo kuanzia kwa mawaziri wake na jeshi la polisi, mfano akiamua kuwatimua kwa kuwa na vitambi tutabaki ka askari si zaidi ya 200 wengi wakiwa FFU maana hao wengi wapo fit.Ria mmoja wa afrika kusini amenyiwa work permit nchini New Zealand kwa sababu ta unene,wabongo tunadhani unene ni afya kumbe ni kifo.Inakuwa mbaya zaidi pale maafande wanaposukuma matumbo,sijui ikiwa huwa wana gwaride hawa jamaa au mazoezi ikiwemo michezo-bia na nyama choma.halafu mkuu wao anadai jeshi lipo gado,bomu moja to chali kwa presha.

    ReplyDelete
  3. Weeee! ofisi yake kumbe huijui. Unaiangalia kwenye picha. Nenda uione live, Ni rais gani anayeweza kuwa simpo? si ndio maana wanagombea nusu kuuana. Unfikiri wanaosema oh uongozi mbovu wana jipya? Hapana ni kutaka kujitutumia... Msemaji wa kwanza hapo umechamka.

    Sata kumwambia mwenzie apunguze kitambi mbele za watu kwanza ni ukosefu wa nidhamu. Huo si uwazi. Baba mzima anaumbuliwa mbele ya kama watoto wake!
    Watu wengine unene ni maumbile.Anataka amkosoe Mungu?

    ReplyDelete
  4. Mdau wa 3 upo sawa kabisa, hapo hakutumia ethics hata kidogo na sijui diplomasia yake ikoje. Angeongea na wahandishi wa habari na wakayaandika kwenye magazeti bila kumtaja mtu! Wakati mwingine ukiwa kiongozi hekima inatakiwa pia kuwa ya hali ya juu. Unene wa asili(genetical) upo na unene wa kujitakia kwa misosi pia upo sasa huu ni shida kubwa sana kwa watu wengi wakimwemo watanzania wengi mno wababa vitambi yani kama wamebeba ndoo za maji tumboni looh! Hakuna mazoezi na ulaji mbaya (unhealthy food). Hebu watanzania tubadilike.

    ReplyDelete
  5. That was very very bad, kama rasi an issue na unene wa jamaa, angemuita chemba akamueleza, Mke hasemwi na Mume mbele ya watoto and vice versa, alitaka amuaibishe tu.On the other hand the guy is morbidly obese.

    ReplyDelete
  6. JK lazima atupie jicho vitambi a.k.a
    vifriji ndani ya jeshi la polisi,magereza,Jkt na JW,vitambi vimekuwa ugonjwa sugu ndani ya vikosi vya ulinzi, utafiti umeonyesha gonjwa wa kufunga minyama ya uzembe umelikumba vikosi vya ulinzi.Ukiwaondoa akina Ras Makunja(FFU) pekee yao ndio hawana vitambi.

    ReplyDelete
  7. Nyie vp?vitambi wenzenu tunavitumia kiulaini kuopoa ng`ashi kitaa.Wenye vitambi flagi kitaa hasa bongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...