Na Mwandishi Wetu
WAREMBO
30 wanaowania taji la Redd’s Miss Tanzania 2013, kesho wanatarajiwa
kukutana rasmi na waandishi wa habari, ili kila mmoja kutoa mtazamo
wake,shughuli itakavyofanyika katika hoteli ya Giraffe iliyopo Kunduchi,
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino ambao ni
waandaaji wa Redd’s Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema, mkutano kati
ya waandishi wa habari na warembo ni muhimu kuwajengea uwezo zaidi wa
kujiamini.
“Washiriki
hao wataulizwa maswali mbalimbali na waandishi wa habari na wao
wataeleza mtazamo wao kuhusu Redd’s Miss Tanzania, hatutawafunga, wao
waandishi watakuwa huru kila mmoja kumuuliza mshiriki yoyote swali
analotaka,” alisema.
Washiriki
hao ambao leo walikuwa na semina maalumu na waandaaji wa mashindano
haya ambao ni Kampuni ya Lino International Agency Limited.
Baada
ya kukutana na waandishi wa habari, warembo hao wanatarajiwa kuanza
ziara maalumu ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa
lengo la kuhamasisha utalii wa ndani.
Warembo
hao watakuwa kambini kwa muda wa siku 30 wakipata mafunzo mbalimbali
yatakayotolewa na wataalamu kutoka katika sekta mbalimbali kama vile
afya, ajira, ujasiriamali, uwekezaji na sekta ya utalii.
Brigitte Alfred ndiye Mrembo anayeshikilia taji hilo kwa sasa, baada ya kufanikiwa kulitwaa mwishoni mwa mwaka jana.
Meneja
wa Redd’s, Victoria Kimaro naye alisema kama wadhamini wapo tayari
kuhakikisha shindano hilo linafanikiwa zaidi mwaka huu kuliko kipindi
chote kile.
Kinywaji cha Redd’s Original kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...