IMG_3248
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jinsi waandaaji wa vipindi wanavyoweza kutafuta habari nzuri zenye kuelimisha kwa ajili ya redio za jamii na pia mbinu wanazoweza kutumia ili kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii.
Akizungumza katika warsha ya siku nne inayoshirikisha waandishi na maripota wa redio za jamii inayofanyika Wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Bi. Ledama ameongeza kuwa upo umuhimu wa kuwajengea uweze watendaji katika redio hizo ikiwemo kuwafundisha namna ya kutumia mtandao wa Intaneti kwa ajili ya kuboresha uandishi na utangazaji , haswa katika maeneo muhimu yanayoigusa jamii ikiwemo Elimu, Afya na Kilimo na pia jinsi redio hizo zinavyoweza kuandaa vipindi vitakavyoigusa jamii moja kwa moja.
Kwa jumla warsha hiyo ya siku nne kwa waandishi wa habari wa redio za jamii imeangalia kwa mapana mambo muhimu ya kijamii, na kuchambua mambo hayo ni yapi ambapo imegusia masuala ya Afya na Kilimo pamoja na mambo mengine na kuangali fursa zinazopatikana, pia changamoto zinazokabili masuala hayo na kutathmini nini kifanyike ili kuboresha utendaji na utoaji huduma katika sekta hizo.
IMG_3079
Mtaalam wa Kilimo kutoka Idara ya Kilimo wilayani Sengerema Bw. Joseph Manota akizungumza katika warsha ya waandishi wa habari wa redio za jamii inayofanyika mkoani Mwanza ambapo fursa zinazopatikana katika sekta ya Kilimo na jinsi ya kuzitumia ili kufanikisha sera ya Serikali ya Kilimo Kwanza na pia amezungumzia changamoto zilizopo katika kutimiza sera hiyo na namna gani maafisa wa Kilimo pamoja na Serikali kwa ujumla wanaweza wakafanya kukabiliana nazo ili kutimiza malengo ya kukuza Kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...