Klabu ya Rotary ya Jijini Dar Es Salaam leo imekabidhi rasmi wodi ya watoto wenye saratani kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wodi hiyo imejengwa na Klabu hiyo kwa kiasi cha Shilingi Billioni 1.2 ikiwa ni gharama za ujenzi, samani, na vifaa tiba vya wodi hiyo. Wodi hiyo ni ya kwanza kwa ubora Kusini mwa Jangwa la Sahara. Tafadhali fuatilia katika picha yaliyojiri wakato wa ufunguzi
Hii ndiyo wodi iliyojengwa na Klabu ya Rotary kwa kushirikiana na wadau wengine. Ni sakafu moja ya juu ambayo imewekwa bango.
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, akifuatiwa na Mgeni rasmi Dr. Jane Goodall aliyeko kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Sr. Agnes Mtawa wote kwa pamoja wakipokea ufunguo wa wodi hiyo kutoka kwa watoto wanaougua saratani.

wageni mbalimbali wakifuatilia kwa karibu hotuba mbalimbali wakati wa ufunguzi.
Wageni wakitembelea wodi kuona ilivyojengwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. safi sana rotary...tungeomba wadau wengine waige mfano huu))

    ReplyDelete
  2. Asante snaa Rotary Club.
    Mimi sina ufahamu mkubwa kwenye mambo ya ujenzi, lakini nimeshtuka ninapolinganisha kiasi cha pesa kilichiotumika hapa na zile zinazotumika kwingine, Bil 1.2 ni pesa nyingi lakini kama hilo jengo lote basi naona kama sehemu zingine wanafanya sarakasi sana. Unasikia zaidi ya bilion 100 zimetumika Benki Kuu, je kweli?

    ReplyDelete
  3. Finally kwenye saratani watoto ni lazima watengwe kabisa na watu wazima wenye saratani. Ashukuriwe aliye juu na wale wote waliohusika kwa hili jambo kufanikishwa. Bado wataalamu sasa waongezeke

    ReplyDelete
  4. Mdau usie fahamu mambo ya ujenzi nami pia kwa matumizi haya sifahamu vizuri,hivyo tupo wengi mno tusiofahamu.Jana nimesoma gazeti moja,linaelezea kisa kimoja kule chalinze ambapo mwalimu mkuu amelazimika kutumia choo kama ofisi kwakua ofisi yake ipo hatarini kuanguka,mwandishi wa habari ile,alisema kwamba vyoo hivyo ambavyo baadhi ya sehemu inatumika kama ofisi kwa huyo mwalimu vilijengwa kama msaada wenye thamani ya milioni 70,yaani nilishindwa kuelewa kabisa iweje ujenge choo huku ukilala nje?hii ni sawa na anaye plani kununua gari kwa kuanza na matairi au usukani,hiyo ndio bongo.

    ReplyDelete
  5. Nawashukuru na kuwapongeza Rotary club kwa kuwezesha ujenzi huu! Hiki ni kitengo nyeti sana kitakacho wa hudumia watoto wetu wa kitanzania na mataifa jirani, hakika mchango wenu huu kwa jamii utakumbukwa daima dumu! Shime kwetu wadau na serikali kukiimarisha, kukitunza na kukiendeleza kitengo hiki ili kitoe tiba stahiki na tarajiwa kwa watoto wetu wenye saratani!

    ReplyDelete
  6. Pongezi kwa walioonesha moyo mwema juo.Jengo ni zuri sasa huduma na mioyo ya matabibu je? Nayo ijengwe upya/ikarabatiwe. Ukienda matibabu India utaona ari ya utendaji wa wafanyakazi hata kama malipo ni hafifu, hapo ndipo tunaposhindwa sisi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...