Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akipata maelezo kuhusu miradi ya maji wilayani Same kutoka kwa mhandisi wa maji wilaya ya Same Musa Msangi.
Naibu waziri wa maji Dk Binilithi Mahenge akiangalia moja ya vilula vilivyojengwa katika kijiji cha Miombo wilayani Same.
Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akiongea na wananchi wa kijiji cha Miombo wilayani Same ambao hata hivyo walidai tangu uhuru hawakuwahi kumuona waziri aliyefika katika kijiji hicho.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mteke wilayani Same Samson Kimbuta akiongea wakati wa mkutano mdogo wa wananchi wa kijiji hicho na naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge aliyetembelea kijiji hicho.
Diwani wa kata ya Mhezi katika kijiji cha Mteke wilayani Same Allen Mbaga kiongea wakati wa mkutano mdogo wa wananchi wa kijiji hicho na naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge aliyetembelea kijiji hicho.
Dk Binilith Mahenge akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mteke wilayani Same wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya maji katika wilaya hiyo. Picha na Dixon Busagaga waglobu ya jamii Moshi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Eti hawajawahi kumuona waziri toka uhuru kuja kututembelea, mie Bibi yangu kule kijijini upareni bado anazani nyerere yupo na bado ni rais.kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  2. Kwenye mradi wa maji wamepanda mikaratusi? sasa hapo si balaa maana hii miti inafyonza sana maji, waing'oe na wapande miti ya asili hasa mikuyu

    ReplyDelete
  3. Dah! Nimepakumbuka sana kwa babu yangu Bombo Mjema!
    Ombe thimanya, nnetonga rini ambu nethina Green card. Yeeuwii nnefwia he ili ithanga la Obama

    ReplyDelete
  4. Kumbe Upareni kuna migomba na ukijani? mie nafikiri ni kama jangwani tu!

    ReplyDelete
  5. Mdau Mwathu hao wanga wanishingha hoi! Hunduka kaa shingha vurundu. Unefwia nyika kididi. Ohoooo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...