KLABU ya Chelsea ya nchini Uingereza,imethibitisha kumsajili mshambuliaji machachari raia wa nchini Cameroon, Samuel Eto’o aliekuwa akikipiga katika klabu ya Anzhi Makhachkala. 

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 imefahamika kuwa amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo kwa dau la pauni milioni 7, japokuwa atapunguziwa mshahara wake kutoka ule wa awali alikuwa akiupata kwenye kbalu ya Anzhi Makhachkala,akiwa ni mchezaji pekee Duniani aliyekuwa akilipwa hela nyingi.ikiwa ni dau la pauni milioni 17 kwa mwaka.

 Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amekata tamaa ya kumshawishi mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney baada ya ofa zake kutupiliwa mbali na Kocha wa Timu hiyo,David Moyes na sasa akaamua kumgeukia nyota wa Kiafrika,Samuel Eto'o.

Mourinho na Eto’o sasa wanakutana kwa mara nyingine,kwani walishawahi kufanya kazi pamoja katika klabu ya Inter Milan na kutwaa kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Samuel Eto'o akiwa na uzi wake alipokuwa akimwaga wino katika Klabu yake mpya ya Chelsea.









Samuel Eto'o akimwaga wino mbele ya Katibu na Mkurugenzi wa Chelsea ,David Barnard.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...