Mpiganaji na mfanyabishara maarufu wa kimataifa "The CEO" Davis Mosha akiongea machache baada ya kukaribishwa kuongea kama kijana mwenye mafanikio na maendeleo kiuchumi, na kijamii wakati wa sherehe za Eid jijini New York. Alitoa ujumbe kwa vijana hasa changamoto za maendeleo zinazo patikana Tanzania. Zaidi Bwana David Mosha amewaasa vijana wa kitanzania kujipatia fedha kwa njia za halali na kusikitishwa sana na wimbi la vijana kujiingiza katika biashara za madawa ya kulevya na nyingine harafu zinazoharibu maisha ya watu na wenyewe kwa ujumla. Mpiganaji Davis Mosha amekuwa Marekani kwa likizo na kila alikokwenda alikutana na watanzania na kuzungumza nao.
David Mosha akisalimiana na waheshimiwa mabalozi..
Waheshimiwa wakikaribishana kwenye meza kuu kwenye sherehe ya Eid Mubarak iliyofanyika 30 Overhill Rd Mt Vernon NY. Sherehe hizo ziliandaliwa na Waislam wa New York na kukaribisha wana jumuia wote pamoja na familia zao bila kujari dini. Hiyo ndiyo dhana tunayojivunia watanzania ya kushirikia katika shughuri za kijamii bila kubaguana Tanzania Oyeeee Mungu ibariki Tanzania.
Katibu wa jumuia ya wataznania New York bwana Shaban Mseba akimuongaza Mgeni rasmi Mh. Balozi Manongi akiwaslri kwenye sherehe hiyo 
Mh. Balozi Manongi akiongea machache mbele ya watanzania waliojitokeza kwenye sherehe hiyo 
Sherehe hizo ziliudhuriwa na mabalozi wetu wote wawili wa hapa New York, Hapa ni Mh. Balozi Mwinyi akiongea kwenye sherehe hiyo.

Hapa ni Mh. Balozi Mero akiongea machache na pia alitumia nafasi hii kuwaaga wananewyork community, Mh. Mero ameteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Geneva na muda wowote ataodoka. 
Katibu wa new York Community bwana Shaban Mseba akiongea
Bwana Hajji Khamis mwenyekiti wa New York Community akitoa shukrani mbele ya watanzania waliojitokeza katika sherehe hizo za Eid Mubarak. Kwa picha bofya read more
Baada ya hivi karibuni kurudi toka safari uko Dubai na Saudia Shekh Maftaha alipata fursa ya kutoa mawahiza katika sherehe hizo za Eid.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Naama Swadaqta Sherehe za Eid zimefana sana huko US.

    Pia Ujumbe wa Masheikh, Waheshimiwa Mabalozi na Ndugu Davis Mosha ni mkubwa sana kwetu!

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Balozi Manongi kwa vazi la mwambao safi sana!

    ReplyDelete
  3. La Muhimu katika Ujumbe mliopewa na Waheshimiwa hao akiwemo ndugu Davis Mosha ni kuwa WATANZANIA TUACHE ILE TABIA MBAYA YA TAMAA ZA UTAJIRI WA HARAKA HARAKA.

    UTAJIRI UNATAKA MIPANGO HUKU MIPANGO NA FURSA ZIKIWEPO NCHINI TANZANIA KAMA MNAVYOONA WAJANJA WA DUNIA MADEGE KILA KUKICHA YANATUA BONGO KWENYE MIPANGO.

    ACHENI KUFIKIRI MAWAZO POTOFU KAMA HAYA KUUSAKA UTAJIRI:

    1.UFISADI.
    2.BIASHARA ZA AJABU KAMA ZA MADAWA YA KULEVYA.
    3.WIZI NA MIPANGO MIPANGO.
    4.UCHAWI KAMA NJIA YA KUUFIKIA UTAJIRI NA MAFANIKIO.
    5.MAJUNGU NA HUJUMA DHIDI YA SISI KWA SISI.

    JAMANI NI AIBU SANA KUPATA MAFANIKIO AMA UTAJIRI KWA NJIA HIZO TANO (5) HAPO JUU.

    KWA KUWA UNAPOPATA MAFANIKIO DUNIA HAINA SIRI LAZIMA ITAJULIKANA UMEFIKIA HAPO KIVIPI?, HIVYO IKIBAINIKA KUTUMIA NJIA ZA MKATO HESHIMA YAKO INASHUKA SANA!

    ReplyDelete
  4. Nchi ya GENEVA Ipo wapi?

    ReplyDelete
  5. Mdau wa 3 umenena na pia Kubwa lao UJAMBAZI Watanzania tuache kazi mbaya na ya aibu ya Ujambazi.

    Tujitahidi kutafuta Utajiri na Fedha kwa njia za halali zaidi!

    ReplyDelete
  6. mbona hakuna waislam kwenye hii shughuli?

    au macho yangu yanatongotongo?

    ReplyDelete
  7. Mdau wa 6 unae uliza hakuna Waislamu kwenye shughuli una uhakika gani kama hao wote hapo HAKUNA KABISA Waislamu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...