Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) linatarajia kufanya mkutano maalum wa kupanga ratiba ya mashindano ya SHIMIWI ya mwaka huu utakaofanyika kesho kutwa jumamosi ya agosti 31 majira ya saa 4 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora zilizopo mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka alisema mkutano huo utawahusisha wenyeviti na makatibu wa vilabu vya michezo ya SHIMIWI kutoka katika Wizara,Idara Zinazojitegemea,Sekretarieti za Mikoa na Wakala za Serikali.
“Wenyeviti na Makatibu wa Vilabu vinavyoshiriki michezo ya SHIMIWI mnatakiwa kuhudhuria mkutano huo bila kukosa ili kufanikisha mashindano ya SHIMIWI yatakayoanza hivi karibuni” alisema Bw.Makuka.
Aidha,Bw.Makuka aliwataka wenyeviti na makatibu wa vilabu vyote kuja na viambatanisho muhimu kama vile barua za kuthibitisha kushiriki,fomu za usajili wa wachezaji watakaoshiriki na vikombe (kwa vilabu vilivyopata vikombe katika mashindano ya mwaka jana yaliyofanyika mjini Morogoro).
Mashindano ya michezo ya SHIMIWI kwa mwaka huu yamepangwa kufanyika mjini Dodoma kuanzia Septemba 21 hadi oktoba 5 ambapo yatahusisha michezo ya mpira wa miguu,netiboli,kuvuta kamba,riadha,baiskeli,karata,bao na drafti.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw.Moshi Makuka akisisitiza umuhimu wa vilabu kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za mashindani ya SHIMIWI leo ofisini kwake.


.png)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...