Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea na moja ya washindi wakati Airtel ilipochezesha droo ya saba ya washindi wa shilingi milioni moja kila siku wa promosheni ya Airtel yatosha ambapo mpaka sasa zaidi ya shilingi million 44 zimeshatolewa. Akishuhudia ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya Bahati nasibu.
Washindi wa siku wa shilingi milioni moja wa promosheni ya Airtel yatosha bwana Thomasi Joackim Chali na Abdallah Omari Muhomba kwa pamoja wakionyesha furaha mara baada ya kukabithiwa zawadi za pesa taslimu baada ya kuibuka washindi wa siku wa promosheni ya Airtel yatosha.

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imetangaza washindi wake saba wa wiki ya saba ya Airtel Yatosha promosheni na kukabidhi zawadi za washindi wa wiki ya sita wa promosheni ya Airtel Yatosha.

Airtel imechezesha droo ya wiki ya saba ya promosheni ya Airtel yatosha Jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco jijini Dar es saalam ambapo wateja saba wameibuka washindi wa kitita cha shilingi million 1 kila mmoja.

Washindi hao ni pamoja na Theresia Martine Komba wa Morogoro -Mkulima, John Kimoro wa kondo Dodoma -Mwalimu, Yohanna Masunga Zengo wa Maswa Shinyanga -Mkulima, Isabellah Joseph wa Chamwino Dodoma -Mwalimu, Nassor Mohammed Nassor wa Kariakoo DSM -Mfanyabiashara, Modest Laurian Mussa wa Bukoba Kagera -Mfanyabiashara na Masanja Mwanamenda wa Nkyala Singida -Mfanyabiashara.

Wakati huo huo Airtel imeendelea kuwazawadia wateja wake kupitia promosheni ya Airtel Yatosha ambapo washindi wa wiki ya sita nao walikabidhiwa zawadi zao ambapo kila mmoja aliondoka na shillingi milioni moja.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo katika ofisi za makao makuu ya Airtel bwana Abdallah Omari Muhomba mmoja wa washindi wa million 1 alisema, "nashindwa jinsi ya kuongea lakini nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kunizawadia shilingi milioni 1 ambazo kwangu nikama ndoto.

Nategemea kutumia pesa hizi kujiendeleza kiuchumi na maaendeleo ya familia yangu. Binafsi nachukua fursa hii kuwaasa watanzania kushiriki katika promosheni hizi za Airtel na kwa hakika wataamka washindi kama mimi hivi leo".

Kwa upande wake bwana Thomas Joachim Chali ambaye pia ni Mshindi wa wiki ya sita alisema, "anawashukuru Airtel kwa kuanzisha promosheni yaAirtel Yatosha , na kuahidi kuzitumia pesa zake kuendeleza na kupanua biashara kwa kuwa hiyo ndio shughuli kubwa anayoifanya".

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo kwa washindi hao Meneja uhusiano wa Airtel bwana Jackson Mmbando alisema, "leo tunao washindi saba waliojishindia shilingi milioni 1 kila moja katika droo ya wiki. Tumeendelea kushuhudia watanzania na wateja wetu wakiibuka mamilionea kila siku na kila mwezi kupitia promosheni hii ya Airtel Yatosha.

Tunaahidi kuendelea kuwazawadia wateja wetu huku tukiboresha huduma zetu , na kuwapata wateja wetu huduma bora zenye gharama nafuu kupitia huduma yetu poa ya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kuwasiliana na mitandao mengine ya simu za mkononi kwa bei poa na kupata vifurushi vya maongezi bila kulipia gharama ya ziada". Aliongeza Mmbando.

Promosheni ya Airtel Yatosha bado inaendelea na wateja wetu wa Airtel Yatosha bado wananafasi ya kuendelea kujishindia pesa taslim na Nyumba mbili za kifahari zilizopo Kigamboni bado kushindaniwa.

Droo itakayomchagua mshindi wa nyumba kwa mwezi huu inatarajiwa kuchezeshwa tarehe 5/9/2013 saa tano asubuhi. hii itachagua mshindi mmoja kati ya wateja wote waliotumia huduma ya Airtel yatosha kwa mwezi huu.

Ili mteja wa Airtel aweze kushiriki anatakiwa kujiunga na vifurushi vya Airtel Yatosha kwa kupiga *149*99# na kujiunga na vivurushi vya Airtel Yatosha. Kila unapojiunga na kifurushi unaingia moja kwa moja kwenye droo ya kushinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...