Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura akiongea wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyekua mwanasheria mkuu wa kampuni hiyo, Bi. Gilder Kibola (kulia) baada ya kustaafu rasmi. Hafla hyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwanasheria Mkuu aliyemaliza muda wake wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Gilder Kibola (kulia) akitoa nasaha zake wakati wa hafla fupi ya kumuaga. Kushoto ni Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni hiyo, Dkt. Kamugisha Kazaura. Hafla hyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Wafanyakazi wa kampuni ya simu Tanzania wametakiwa kuongeza juhudi, umoja na maarifa katika kazi zao ili kuhakikisha wanaifanya kampuni hiyo kuwa mfano wa kuigwa ndani na nje ya nchi.

Wito huo umetolewa na aliyekua mwanasheria mkuu wa kampuni hiyo, Bi. Gilder Kibola alipokua akiongea na wafanyakazi wenzake na uongozi wa kampuni hiyo katika hafla fupi ya kumuaga mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam baada ya kustaafu.

Bi. Kibola alisema ni muhimu kwa wenzake wanaobaki kuendeleza juhudi na kumpa kila aina ya ushirikiano Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo kufikia malengo ya kampuni.

“Mzidi kumpa ushirikiano kiongozi wetu ili malengo yaweze kufikiwa,” alisema. Bi. Kibola alisema kuwa kufaniksha mipango na malengo ya kampuni hutegemea sana ushirikiano na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu miongoni mwa wafanyakazi katika kampuni.

Bi. Kibola alijiunga na kampuni hiyo mwaka 1996 akiwa kama afisa sheria na kupanda ngazi hadi kufikia hapo wakati wa kustaafu kwake.

“Ninashkuru Mungu…namaliza salama na afya njema, nimejifunza mengi sana,” anasema. Aliwaomba vijana katika kampuni hiyo kuhakikisha wanajifunza kwa waliowatangulia utendaji kazi mzuri kwa kuzingatia busara na weledi.

“Jifunzeni kwa watu waliowatangulia kazini, mtafanikiwa,” alisema.

Afisa Mkuu Mtendaji wa TTCL, Dkt. Kamugisha Kamuzora alisema kampuni itamkumbuka hasakwa ucheshi, uchapa kazi na weledi wake,” alisema.

“Tutakukumbuka…lakini faraja yetu ni kuwa umeacha nyuma timu imara ambayo ulishiriki kuitengeneza,” alisema.

kwa upande wake meneja wa sheria wa kampuni hiyo, Bi. Lugano Rwetaka alisema kuwa watakumbuka na kuthamini mchango wake katika kiuongoza na kuishauri kampuni katika masuala mbalimbali ikiwemo mikataba,utoaji wa tenda, na masuala mbalimbali ya kisheria. “Utendaji wako ulikua ni kwa sifa yako pamoja na idara ya sheria…umetujengea uwezo ambao tutaendelea kuutumia kujenga kampuni,” alisema.

Mkuu wa utumishi wa Kampuni hiyo, Bw. Juvenal Utafu alisema Bi. Kibola amekua pamoja na kampuni katika vipindi mbalimbali vilivyopitiwa na TTCL na hakutetereka hadi anastaafu kwa heshima.

“Alikuwa ni kiungo muhimu kati ya wafanyakazi na bodi na amechangia mafaniko katika idara ya sheria,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. HONGERENI VJANA KWA UCHAPAJI KAZI MZURI NAWATAKIA MAFANIKIO NA TAIFA KWA UJUMLA, HONGERA DR KAZAURA NAJUA KAMA NIWEWE NINAEFIKIRIA NI MTOTO WA BALOZI KAZAURA BASI NIJEMBE ZURI MAANA UTAKUA UMERITHI KWA BABAYAKO MAANA NIMCHAPA KAZI MZURI SANA BIG UP DR KAMUGISHA. SALAMU KWA FAMILIA YOTE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...